Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi
la Polisi Mstaafu Omar Mahita Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Cornel Lundu Apson mara baada ya mazungumzo yake na viongozi wastaafu na wa sasa wa vyombo vya Ulinzi na Usalama Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi wa vyombo vya Ulinzi
na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Omar Mahita(IGP Mstaafu), Said Mwema(IGP
Mstaafu) pamoja na Ernest Mangu(IGP Mstaafu) Ikulu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wasasa
na wastaafu wa Magereza Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na na viongozi
wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam
mara baada ya mazungumzo yao.
*****************
RAIS Dkt. John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wastaafu na
viongozi wa sasa wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini, Ikulu jijini Dar
es Salaam leo.
Viongozi
hao ni Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Wakuu wa Jeshi
la Polisi, Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Wakuu wa Idara ya Uhamiaji,
Wakuu wa Jeshi la Magereza na Wakuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Baada
ya mazungumzo hayo viongozi wastaafu wa vyombo vya ulinzi na usalama
wamemshukuru Rais Magufuli kwa kuwaita na kufanya nao mazungumzo, ambayo
yamewawezesha kubadilishana mawazo na kuimarisha zaidi ushirikiano kati yao na
viongozi wa sasa wa vyombo hivyo.
“Tunamshukuru
sana Rais Magufuli na tunampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya, sio jambo la
kuficha amefanya kazi nzuri, na kila mmoja wetu amezungumza hilo na tunamtakia
kila la heri ili aweze kuendeleza pale alipofika, kwa kweli tumefurahi sana,”
amesema Cornel Apson, Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa Mstaafu.
“Tumeona
ni jambo jipya na halijawahi kutokea kwa Rais kutuita viongozi wastaafu, nchi
yetu chini ya Mhe. Magufuli inakwenda vizuri, Watanzania tuiunge mkono Serikali
hii kwa sababu inatuelekeza mahali kuzuri,” amesema Jenerali Mstaafu Robert
Mboma, Mkuu wa JWTZ Mstaafu.
Viongozi
hao wamempongeza, Rais Magufuli kwa uendeshaji mzuri wa Serikali, hususani
katika kusimamia uchumi, kupiga vita rushwa, kujenga nidhamu kwa watumishi wa
umma na wamemuahidi kuendeleza zaidi ushirikiano na viongozi waliopo sasa.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu , erson Msigwa amesema Rais Magufuli amekutana na
viongozi hao kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujenga ushirikiano imara
zaidi kwa viongozi wastaafu na viongozi wa sasa katika kutekeleza majukumu ya
ulinzi na usalama wa nchi.
“Rais
Magufuli amefurahishwa sana na mwitikio wa viongozi hawa wastaafu wa vyombo vya
ulinzi na usalama na amewahakikishia kuwa Serikali anayoiongoza itaendeleza
ushirikiano nao ili kunufaika na uzoefu wao,” amesema Msigwa
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment