Waokoaji wakiwanasua wachimbaji kutoka katika kifusi kilichowafunika ardhini.
Wachimbaji wakiwa wameokolewa na wakipatiwa huduma ya kwanza.
Jopo la Madaktari na wauguzi wakiendelea kuwapa huduma.
Watu wa 15 waliofukiwa na kifusi katika mgodi wa Dhahabu wa RZ Nyarugusu mkoani Geita, wameokolewa hai.
Leo asubuhi timu ya waokozi ilitoboa shimo hadi eneo walilokwama watu hao na kutumbukiza tochi na redio ya mawasiliano kwa kutumia kamba na ikarudi juu ikiwa tupu. "Tumeshusha tochi na radio via drill hole ,kamba ikarudi tupu means vimepokelewa lakini kwenye radio awasikiki," ilisema taarifa kutoka eneo la tukio.
Aidha waokoaji walishusha barua peni na karatasi kupitia shimo hilo na vitu hivyo vikapokelewa na kurejesha majibu kuwa wote 15 wazima isipokuwa mmoja amechomwa na msumari na kuorodhesha majina yao nankuimba chakula.
Timu ya madaktari walishauri wasipewe chakuka bali dripu tu wanatakiwa wanywe mana awajala siku mbili.
Kwa sasa zinashushwa dripu maalum za maji kupitia shimo hilo.y
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment