Waziri
wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amemuagiza Msajili wa vyama vya Siasa
kuchukua hatua kwa vyama vinavyokiuka sheria na miongozo ya vyama vya siasa.
Ametoa
kauli hiyo leo (Aprili 23, 2018) alipokuwa akitoa maelezo ya ufafanuzi juu ya hoja
za ofisi yake, zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti na Ukaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018 alipokutana
na waandishi wa habari Bungeni Dodoma.
Waziri
Mhagama ameelekeza kuhakikisha vyama vyenye mapungufu upande wa hesabu zao basi
wawasilishe kwa Msajili wa vyama ndani ya wiki 3 hadi 4.
“Namtaka
Msajili wa Vyama achukue hatua za Kisheria pasi kusita kwa chama chochote
kinachokiuka sheria ya vyama vya siasa Na. 2 ya mwaka 1992”.alisema Waziri
Mhagama
Aidha
amemtaka Msajili wa Vyama vya siasa nchini kuhakikisha anaweka miongozo na
mpango kazi ili vyama vilivyozoea kutowasilisha hesabu zao viache mara moja kwa
mujibu wa sheria.
Waziri
Mhagama aliongezea kuwa taarifa ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali ilibaini mapungufu kadhaa katika uendeshaji wa vyama vya siasa
ikiwemo; Upungufu katika hesabu zilizowasilishwa chini ya viwango vya Kimataifa
vya uandaaji wa hesabu katika sekta za umma na baadhi ya vyama kushindwa
kuwasilisha hesabu zao kwa CAG kwa ukaguzi
Pamoja
na hayo alibainisha kuwepo kwa vyama vya kisiasa visivyotumia rejista ya mali
za kudumu ambapo vyama vinne ikiwemo;CHADEMA, NLD,ADC na Demokrasia Makini
havina Daftari la kudumu la mali zao ikiwa ni kinyume na sheria zilizopo.
“Msajili
wa Vyama nakuagiza kutoa maelekezo kwa kila chama cha siasa chenye usajili wa
kudumu kuwa na regista ya mali zake ndani ya wiki tatu kuanzia leo kwani kukosa
daftari la mali za kudumu ni kinyume na kifungu Na.14(1)(b)(ii) ya sheria ya
vyama vya siasa Na.5 ya mwaka 1992.”alisisitiza Waziri.
Sambamba
na hilo Waziri alimtaka Msajili wa Vyama vya siasa kuhakikisha vyama vyote vinafuata miongozo yote ya kihasibu ili
kuondokana na mapungufu ya kukosekana kwa nyaraka za malipo kama
ilivyobainishwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambapo alibaini vyama
vitatu kati ya tisa vina nyaraka pungufu ikiwemo CHADEMA, SAU na ADC.
“Msajili
wa vyama ahakikishe vyama vya siasa vinatekeleza miongozo yote kihasibu pamoja
na kanuni za fedha, ambazo zinaelekeza nyaraka ziwe na viambatisho sahihi kwani
ripoti ilibainisha vyama vitatu vilikuwa na malipo yenye nyaraka pungufu zenye
thamani ya shilingi 735,978,559 ambapo ni kinyume na miongozo ya kihasibu na kukosa
uhalali wa malipo hayo.”alisisitiza Waziri Mhagama.
AWALI:
Kifungu cha 14(1)(a) na (b)(i) cha Sheria ya
Vyama vya Siasa Sura ya 258 [RE: 2015] kinaelekeza kuwa, kila chama cha siasa
kinapaswa kutunza taarifa za mapato na matumizi, ikiwamo taarifa za mali zake.
Vile vile, kinapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, taarifa ya
hesabu zake zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG), pamoja taarifa ya mali zake.
Hivyo, Kifungu hicho kinampa mamlaka Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi wa hesabu za kila chama cha
siasa chenye usajili wa kudumu. Katika mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni,
2017, CAG amefanya ukaguzi wa hesabu za Vyama vya Siasa kumi ikiwemo; CCM, CHADEMA, NLD, TLP, Demokrasia
Makini (MAKINI), TLP, DP, SAU, AFP, CCK na ADC kati ya
vyama vya siasa kumi na tisa vyenye usajili wa kudumu. Vyama vya Siasa tisa (9)
havikuwasilisha hesabu zake kwake kwa wakati kwa ajili ya ukaguzi, hivyo
hakukaguliwa.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment