Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akimkabidhi cheti mmoja ya
wahitimu wa kozi fupi katika chuo cha michezo Malya hivi karibuni.
(Picha na Habari vyote na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza).
Catherine Laurence, akisoma Risala kwa Niaba ya wanafunzi wenzake wakati wa mahafali ya kozi fupi chuo cha Michezo Malya.
***********
Na Atley Kuni, Mwanza
Serikali imesema itakuwa bega kwa bega na Chuo cha michezo Malya ili
kuhakikisha chuo hicho kinakuwa kitovu cha kuzalisha walimu bora na wenye
weledi katika masuala mazima ya michezo hapa nchini na hata nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, alipokuwa akifunga mafuzo ya muda mfupi
yanayo tolewa na chuo hicho, ambapo jumla ya wahitimu wapatao sitini na tisa
(69) walitunukiwa vyeti na waziri huyo.
Dk Mwakyembe amesema, kama wizara, nilazima wakifanye chuo cha Michezo
Malya kuwa “Strategic thinking” kwa maana ya stratejia ya wavumbuzi wa vipaji
vya watu wa kada mbali mbali hususan katika suala zima la walimu wa michezo “Nilipo
tembelea na kukiona chuo nimepata picha kamili ya chuo hiki, hii sasa inanipa
shauku yakuwashauri muandae dira endelevu kwa chuo chetu” alisema Mwakyembe.
Dk Mwakyembe, amesema katika Ibara ya 161 (G) ya Ilani ya Chama cha
Mapinduzi ya 2015-2020, inaweka bayana na kutia msukumo wa masuala ya michezo,
lakini pia Rais wa Jamhuri ya Muungano ameonesha dhamira ya dhati katika hilo
hata mbele ya Mataifa mengine ndio sababu Morocco, wanataka kujenga ‘Sport
Complex’ Makao Makuu ya nchi Dodoma.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho, amesema katika kuhakikisha chuo
hicho kinafanya vema katika siku za usoni wamedhamiria kuongeza idadi ya kozi
zitakazo kuwa inatolewa kwa wakurufunzi wanaotaka kujiunga na chuo hicho
ukiwepo mchezo wa Whushu ambapo China kupitia ujumbe
wake iliowakilishwa na Bi. Amber, uliozulu chuoni hapo wakati wa mahafali,
umeonesha nia yakuleta walimu wa Whushu.
Mbali na jukumu la kuongeza aina ya kozi zitakazo tolewa na chuo hicho
kwa ngazi ya Stashahada (Diploma) mkuu huyo amemweleza waziri changamoto zinazo
kikabili chuo hicho ambazo nipamoja na uhaba wa maji, Gym ya mazoezi, hali
inayosababisha timu mbali mbali za mpira wa miguu zinazo tamani kwenda kuweka
kambi katika eneo hilo kushindwa kutokana na ukosefu wa Gym, “Mh. Waziri
ilikuja timu ya Mbao FC, kilio chao kikubwa ilikuwa ni eneo la Mazoezi ya
viungo (Gym Fitness centre)” alisema mkuu huyo wa chuo.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Michezo nchini Dkt. Yusuph Singo
Omary, kutoka Wizara ya habari, amesema hivi sasa Serikali ipo katika mchakato
wa kutenga shule 55 ikiwa ni hatua itakayo saidia katika kukuza na
kuendeleza vipaji vya michezo nchini kuanzia vijana wanapokuwa wadogo.
Awali akimkaribisha Waziri wa habarikuzungumza katika mahafali hayo,
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Mtemi Msafiri, alimuomba waziri, Wizara ya
habari kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na TAMISEMI, kuona Umuhimu
wakukisaidia chuo hicho katika kukiendeleza, “Tunaomba Mhe. Waziri ili chuo
hiki kiweze kwenda mbele basi vema kila Halmashauri ikaagizwa kugharamia angalau
Walimu wawili kila mwaka”, alisema Msafiri na kuongeza kuwa endapo Halmashauri
zote nchini 189, zikileta walimu wawili tu basi tutakuwa na wanafunzi 378, hii
itakisaidia chuo chetu kukua zaidi, lakini pia kupata walimu wenye weledi.
Kwa upande wao wahitimu hao wamemuomba waziri kupewa kipaumbele katika
Michezo ya UMISETA na UMITASHUMTA, Akisoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake
Catherine Laurent, amesema wao wamejifunza Sheria na kanuni za Michezo mbali
mbali kwa kipindi chote walichokuwepo chuoni hapo hivyo wanaomba kupewa
kipaumbele katika kufundisha michezo pindi warejeapo kwenye vituo vyao vya kazi
kwani sasa wanatambua sheria, kanuni na taratibu zinazo ongoza michezo waliyo
jifunza.
Chuo cha michezo Malya kilianzishwa mwaka 1979, kikiwa na lengo la
kufundisha na uendeleza walimu wa michezo katika ngazi ya Astashahada na badae
mwaka 1995, ndipo kilianza kuzalisha walimu wanafunzi wa ngazi ya Stashahada
(Diploma). Lakini pia kimekuwa kikiendesha kozi fupi za wiki mbili ambazo
huwajengea uwezo wahusika kabla yakuendelea na ngazi ya Diploma.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment