Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday 27 June 2017

BALOZI DK NCHIMBI AKABIDHI HATI YA UTAMBULISHO KWA RAIS TEMER WA BRAZIL

BALOZI wa Tanzania nchini Brazili, Dk. Emmanuel Nchimbi amewasilisha hati ya uteuzi wake kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Brazil, kwa Rais wa nchi hiyo, Michel Temer. Anaandika Mroki Mroki.


Balozi Dk Nchimbi alisuindikizwa na maofisa kadhaa wa ubalozi wakati wa kukabidhi hati hiyo.

Itakumbukwa kuwa Dk. Nchimbi aliteuliwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, mnamo Desemba 3, 2016 kuwa Balozi, ambapo katika uteuzi huo jumla ya Mabalozi 15 waliteuliwa.

Mwezi Januari mwaka huu Rais Magufuli aliwapangia kazi mabalozi wapya saba kati ya Mabalozi 15 aliyowateuwa kujaza nafasi zilizo wazi katika Balozi za Tanzania zilizopo katika nchi mbalimbali. 

Miongoni mwa Mabalozi hao wapya waliopangiwa vituo vya kazi ni pamoja na Balozi Mbelwa Brighton Kairuki wa Tanzania Beijing – China China, Balozi George Kahema Madafa wa Tanzania Rome–Italy na Balozi Emanuel John Nchimbi wa Tanzania Brasilia – Brazil.

Wengine katika Orodha hiyo alikuwepo, Balozi Fatma Rajabu wa Tanzania Doha – Qatar, Balozi Prof. Elizabeth Kiondo wa  Tanzania Ankara – Uturuki na Balozi Dkt. James Alex Msekela wa  Tanzania Geneva – Umoja wa Mataifa.

 Balozi wa Tanzania nchini Brazili, Dk. Emmanuel Nchimbi aakisalimiana na Rais  Brazil Michel Temer.
Balozi Dk Nchimbi akiwa katika picha ya Pamoja na Rais wa Brazil na maofisa wa pande hizo mbili wakati wa kuwasilisha hati ya uteuzi kutoka kwa Rais Dk. John Magufuli.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment