Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Aprili 2017, amekutana
na kuzungumza na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali na kuuagiza viongozi wa
mkoa wa Kilimanjaro kutatua kero zinazowakabili wananchi wa mkoa huo.
Rais Magufuli
ametoa agizo hilo kufuatia malalamiko ya baadhi ya viongozi wa dini kueleza
kero zinazowakabili ikiwa ni pamoja na manyanyaso yanayofanyiwa na wafanyakazi
wa Wakala wa Maegesho ya magari mkoani humo.
Kufuatia malalamiko
hayo, Rais Magufuli amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa nchini TAKUKURU kuchunguza mkataba uliongiwa kati ya Manispaa ya Moshi
na Wakala wa Maegesho ya magari mkoni humo ili kujua uhalali wake kwani
kumekuwa na ubadhirifu mkubwa wa upotevu wa mapato yatokanayo na makusanyo ya
maegesho hayo.
'' Uangalie ule
mkataba wa parking wa hapa Moshi,kama kuna ufisadi wowote peleka Mahakamani,lakini
haya ya administration kayaangalie wasinyanyase watu, huwezi hata ukamuona
sheikh unafunga gari lake,ukimuona Mchungaji na kola yake unafunga tu ni
ushetani,sasa saa nyingine wale vijana wanaofanya ile kazi wanajisahau, hawaheshimu
utu wa Watanzania'' amesema Rais Magufuli.
Pia amemuagiza Mkurugenzi
wa Manisapaa ya Moshi kutoa kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Uchunguzi wa maradhi
kilichoombwa na mwananchi mmoja mkoani humo ili aweze kuendelea na ujenzi huo kutokana
na kutopewa kibali hicho kwa muda mrefu.
Katika
hatua nyingine, Rais Magufuli amesema kutokana na Serikali kuzuia unywaji wa pombe
aina ya viroba idadi ya vifo katika mkoa wa Pwani imepungua kutoka 80 hadi 20
na hata ajali za pikipiki maarufu Bodaboda nazo zimepungua nchini.
Aidha, Rais
Magufuli ametaka uongozi wa Wilaya ya Hai kufanya kazi bila kutishwa na
madiwani ikiwa ni pamoja na kubadili sheria ndogondogo wilayani humo ili
kupunguza kero za utitiri wa ushuru kwa wananchi.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo wakati alipokutana
na viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro, Vyama vya Siasa na watendaji wa
Serikali mkoani humo na kula nao chakula cha mchana kilichoandaliwa na mkoa wa
Kilimanjaro.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment