Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole
**********
Na
Katuma Masamba
CHAMA
cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimeridhishwa na uamuzi wa Rais John Magufuli wa kuzia
mchanga wa madini (Makinikia) kwenda nje ya nchi ikiwa ni hatua ya kulinda
rasilimali za Watanzania.
Aidha,
Chama hicho kimezipongeza kamati mbili zilizokuwa zikiongozwa na Profesa
Abdulkarim Mruma na Profesa Nehemiah Osoro zilizoundwa kwa ajili ya uchunguzi
wa mchanga wa dhahabu uliokuwa ukisafirishwa kwenda nje ya nchi kwa uzalendo wa
kweli ambao licha ya kuwepo kwa vitisho na hongo lakini zilisimama kwa ajili ya
kulinda maslahi ya Watanzania.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole wakati
akizungumza na vyombo vya habari leo (Alhamisi) katika Ofisi ndogo za Makao
Makuu ya chama hicho zilizopo Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Amesema
kilichofanywa na Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM ni kuanza kuweka
mifumo ya kusimamia na kukomesha utoroshwaji wa mali ya Watanzania, hatua
ambayo ni sehemu ndogo ya mambo mengi ambayo yameshatekelezwa yaliyomo katika
ilani ya chama hicho.
“CCM
imefurahishwa na uamuzi wa Rais haukuwa uamuzi mrahisi haukuwa uamuzi mwepesi
na mi nadiriki kusema kulikuwa n amashinikizo makubwa sana, lakini
tumefurahishwa na msimamo dhabiti na madhubutu wa Rais na timu yake,” amesema
Polepole.
Aidha,
ameelezwa chama hicho kuridhishwa na hatua ya awali ya Mwenyekiti wa Kampuni ya
Barrick Gold Corporation ya Canada, Profesa John Thornton kuja kukutana na Rais
Magufuli na kukubali kulipa fedha zote.
Polepole
pia ametaka agizo la Rais Magufuli la kuchunguzwa kwa watu wote waliohusika,
huku akitaka watu hao kutoa ushirikiano ili ujulikane ukweli ujulikane kwakuwa
chama hicho kinataka kuona Watanzania wananufaika na rasilimali zao.
Amesema kitendo
cha Rais Magufuli kuzuia maslahi ya watu wakubwa na mashirika makubwa kinahitaji
moyo mkubwa wa kujitoa na wakizalendo kama alionao Rais Magufuli. Polepole pia
alikiri kuwa yapo makosa yalifanyika kipindi cha nyuma lakini nkwa sasa chama
hicho kinaanza upya kwa kuwa Watanzania wanataka kiwe kisafi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment