Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Thursday, 15 June 2017

UTAFITI: CCM YAENDELEA KUKUBALIKA UKILINGANIOSHA NA CHADEMA

KUKUBALIKA kwa vyama vya siasa kunatoa taswira mchanganyiko ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuimarika, ikiwa ni kati ya asilimia 54 na asilimia 65 kati ya mwaka 2012 na 2017.

Baada ya kushuka mwaka 2013 na 2014 ambapo kiwango cha kukubalika kilifikia asilimia 54 kutoka asilimia 65 ya 2012. Kukubalika kwa CCM kumeendelea kubaki katika kiwango hicho hicho cha asilimia 62 tangu uchaguzi wa mwaka 2015 na asilimia 63 mwaka 2017.

CCM inakubalika zaidi miongoni mwa wazee ikiwa ni sawa na asilimia 80, ukilinganisha na asilimia 55 ya vijana. Wanawake kwa asilimia 68 wanaikubali CCM kuliko wanaume wenye asilimia 58.

Maeneo ya vijijini  wanaikubali kwa asilimia 66 kuliko maeneo ya mijini yenye asilimia 57 na wananchi masikini asilimia 69 kuliko matajiri asilimia 53.

Wananchi wenye elimu ya sekondari, elimu ya ufundi au elimu ya juu wanaikubali CCM kwa asilimia 46.
Kukubalika kwa Chama chja Demokrasia na maendeleo (Chadema) kumeshuka hadi asilimia 17 mwaka 2017 kutoka asilimia 32 mwaka 2013.
Kukubalika kwa Chadema kwa ujumla unafuata mtiririko tofauti: ni mkubwa miongoni mwa vijana, wanaume, watu matajiri na wenye kiwango kikubwa cha elimu.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika utafiti wake uitwao Matarajio na matokeo; Vipaumbele, utendaji na siasa nchini Tanzania.

Utafiti huo unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi.


Matokeo hayo yanatokana na takwimu zilizokusanywa mwezi Aprili mwaka 2017 kutoka kwa wahojiwa 1,805 kutoka maeneo mbalimbali Tanzania Bara 


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment