ASILIMIA 71 ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais John Magufuli tangu
alipoingia madarakani.
Rais anakubalika zaidi miongoni mwa makundi ya wazee na wenye kiwango
kidogo cha elimu
Kiwango
hiki kimeshuka kutoka asilimia 96 mwezi Juni 2016. Viwango vya kukubalika
kwa Rais vinatofautiana katika makundi mbalimbali ambapo asilimia 68 wenye umri
chini ya miaka 30 wanamkubali Rais Magufuli ikilinganishwa na asilimia 82 wenye
umri zaidi ya miaka 50.
Aidha
asilimia 75 ya wananchi wenye elimu ya msingi au chini yake wanamkubali Rais Magufuli
ikilinganishwa na asilimia 63 ya wale wenye elimu ya sekondari au zaidi na asilimia
75 ya wananchi masikini wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 66 ya
wananchi matajiri.
Wakati
viwango hivyo kukubalika kwa Rais vikionesha kushuka ukilinganisha na utafiti
wa mwezi Juni mwaka jana, viwango vya kukubalika kwa viongozi wengine navyo pia
vimeshuka katika kipindi hicho hicho.
Utafiti
unaonesha kuwa Wabunge kukubalika kwao
kiutendaji kumeshuka kutoka
asilimia 79 ya mwezi Juni 2016 hadi
asilimia 58 ya Aprili 2017 huku Madiwani
kukubalika kwa utendaji wao ukishuka kutoka asilimia 74 Juni 2016 hadi asilimia
59 ya Aprili 2017.
Kundi lingine
la viongozi wa wananchi ni la Wenyeviti wa vijiji/mitaa na vitongoji ambalo Kukubalika kwao kiutendaji kumeshuka kutoka
asilimia 78 Juni 2016 hadi asilimia 66 ya Aprili 2017.
Matokeo
haya yametolewa na Twaweza katika utafiti wake uitwao Matarajio na matokeo;
Vipaumbele, utendaji na siasa nchini Tanzania.
Utafiti
huo unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani
Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi.
Matokeo
hayo yanatokana na takwimu zilizokusanywa mwezi Aprili mwaka 2017 kutoka kwa
wahojiwa 1,805 kutoka maeneo mbalimbali Tanzania Bara
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment