Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday 26 April 2017

MANISPAA YA ILALA YAWAKUMBUKA WAKAZI WA MAJOHE YAANZA UJENZI WA BARABARA YAO



Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amezindua rasmi ujenzi wa barabara ya kilometa saba kutoka Pugu hadi Majohe ili kuondoa kero ya kushindwa kupita barabara hiyo hasa katika kipindi hiki cha mvua.

Mjema amezindua barabara hiyo leo ambapo pia ameagiza kuvunjwa kwa nyumba zaidi ya 10,zilizojengwa katika Bonde la Viwege Dampo katika Kata ya Majohe.

"Nyumba zote zilizoko hapa ziwekewe X kwa kuwa ziko bondeni na ninaagiza eneo hili kusiendelee ujenzi wa aina yoyote kwa sababu ni eneo hatarishi. Hatuwezi kuhatarisha maisha ya wananchi wengi, kwasababu ya watu wachache," amesema Mjema.

Amesema atahakikisha barabara hiyo inatengenezwa kwa kiwango cha chanagarawe na kukamilika katika kipindi cha miezi mitatu hivyo wananchi wawe wavumilivu katika kipindj ambacho barabara hiyo inatengezwa


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment