Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk Charles Mlingwa, akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mara hii leo kuhusiana na mkoa huo kuwa mwenyeji wa siku ya mazingira.
****************
MKOA
wa mara umechaguliwa kuwa mwenyeji wa Siku ya mazingira duniani ambapo kitaifa itaadhimishwa
kitaifa mkoa wa Mara katika Wilaya ya Butiama kuanzia Juni 1-6 mwaka huu.
Waziri
katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Januari Makamba
anataraji kufungua maadhimisho hayo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan
anataraji kuwa mgeni rasmi katika kilele chake.
Maadhimisho
hayo yatafanyika katika uwanja wa Mwenge Mjini Butiama ambapo kutakuwapo na kongamano
na tafrija mbalimbali kuhusiana na maswala ya mazingira.
Mkuu
wa mkoa wa Mara, Dk Charles Mlingwa alisema kuwa katika siku hiyo ya mazingira
inategemewa kupandwa miche ya asili 1,500 ya miti katika misitu mbalimbali eneo
la Butiama kama ilivyo kawaida ya maadhimisho hayo.
Aidha
Dk Mlingwa amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi ili kujumuika pamoja kwenye maadhimisho
hayo muhimu ambayo yatafanyika mkoani Mara kwa mara ya kwanza.
Mbali
na hapo Mlingwa alisema kuwa wananchi watapata faida katika maadhimisho hayo
kama kuijengea jamii uwezo juu ya uelewa wa masuala ya mazingira na changamoto
za kijamii zinazojitokeza katika utunzaji wa mazingira na kuwezesha wadau
kushiriki katika fursa zinazohusiana na upandaji wa miti.
Pia
watapata fursa ya kujadili mwendelezo wa utekelezaji wa shughuli zilizoratibiwa
katika mkoa na wizara kuhusu namna bora ya uhifadhi wa mazingira na kuenzi kazi
zote za Baba wa Taifa Mwal. Julius Nyereree katika hifadhi ya mazingira.
Mlingwa
alisema kuwa wataelimishwa kupanda miti ili kukidhi mahitaji ya dunia ya
kupambana na ongezeko la hewa ya ukaa.
Kaulimbiu
ya mwaka huu ni “Hifadhi mazingira muhimili wa Tanzania ya viwanda” ikiwa na
maana ya ulinzi na uhifadhi wa mazingira nchini kuleta maendeleo endelevu ya
kiuchumi na kijamii.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment