Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday 30 May 2017

UPEPO MKALI WA KASI YA KILOMETA 40 KWA SAA WATARAJIWA KUVUMA PWANI YA TANZANIA

UPEPO mkali wa kusi wenye kasi ya kilometa 40 kwa saa unataraji kuvuma utasababisha mawimbi yenye ukubwa wa mita 2 baharini.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa tahadhari ya kuwepo kwa upepo huo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya pwani ya Tanzania.

Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba huko Kisiwani Zanzibar ndivyo vitakubwa zaidi na upepo huo.

"Msukumo wa upepo wa Kusi unatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika ukanda wa pwani ya Tanzania," Ilisema taarifa ya TMA.

Tahadhari kubnwa imetolewa kwa wavuvi na watumiaji wengine wa bahari hasa maeneo yaliyotajwa ili kuepuka ajali ambazo zinaweza kuepukika.

Hali hiyo ya hewa inatarajiwa kuwepo hadi kufikia kesho 31 Mei,2017.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment