Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Thursday, 27 July 2017

RAIS ASISITIZA WASIOENDELEZA VIWANDA MOROGORO WAVIREJESHE SERIKALINI

Rais Dkt John Magufuli Akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia Wananchi wa eneo la Stendi ya Mabasi Msamvu  Mkoani Morogoro akitokea Mkoani Dodoma leo Julai 27,2917 na kutoa maagizo kadhaa.


RAIS John Magufuli amewataka watu wote waliobinafsishiwa viwanda mkoani  Morogoro kuvirejesha Serikalini endapo wameshindwa kuviendeleza ili wapewe wawekezaji wanaoweza kuviendeleza na kuzalisha ajira.

Rais Magufuli ametoa wito huo leo wakati baada ya msafara wake uliokuwa ukitoka Dodoma kuelekea Jijini Dar es Salaam kusimamishwa na wananchi wa Morogoro katika eneo la Msamvu mjini humo.

“Ninarudia wito wangu niliokwisha kuutoa huko nyuma, kwamba wenye viwanda hapa Morogoro ambao wameshindwa kuviendesha, na leo nataja akiwemo Mbunge wa hapa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), narudia akiwemo Mbunge wa hapa wa CCM ambaye alibinafsishiwa viwanda vingi, kama ameshindwa kuviendesha avirudishe ili tuwape watu wengine kwa sababu vijana hawa wanakosa ajira, nazungumza kwa uwazi kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu” amesisitiza ,  Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amewaagiza viongozi wa Manispaa ya Morogoro na viongozi wa Mkoa wa Morogoro kuwaacha wafanyabiashara ndogondogo wa Mji huo waendelee kufanya biashara zao katika eneo la kituo cha mabasi cha Msamvu mjini humo hadi pale utaratibu mzuri utakapowekwa.

Alisema hayo baada ya wananchi wa Morogoro katika eneo la Msamvu kumueleza kero ya kunyanyaswa na Manispaa ambao wamekuwa wakiwafukuza katika maeneo wanayofanyia biashara hasa baada kituo cha mabasi cha Msamvu kujengwa upya.

Magufuli amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro SACP - Ulrich Matei kuhakikisha Askari Mgambo hawawasumbui wafanyabiashara ndogondogo na amewataka wafanyabiashara hao kutofanya vurugu wakati utaratibu mzuri unaandaliwa kwa ajili yao.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewapongeza wakulima wa mazao Mkoani Morogoro kwa kuongeza uzalishaji wa mazao na amewataja wakulima wa Wilaya ya Kilosa kwa kuongeza uzalishaji kutoka asilimia 42 msimu uliopita hadi kufikia asilimia 82 katika msimu huu.

Kuhusu mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) Rais Magufuli ametoa wito kwa wananchi wa Morogoro kujitokeza kupata ajira wakati wa ujenzi, lakini amewataka waliojenga katika hifadhi ya reli kuondoa majengo yao kwa hiari.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment