“Kwa
masikitiko nimepokea taarifa za kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini, Mzee wangu Philemon Ndesamburo kilichotokea leo tarehe 31
Mei, 2017 katika hospitali ya rufaa ya KCMC iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro,
Namkumbuka Mzee Ndesamburo kwa hekima zake na uongozi wake uliozingatia siasa
za kistaarabu”
Hii
ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli aliyoitoa katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya Marehemu
Philemon Ndesamburo, Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) pamoja na ndugu, jamaa na
marafiki wote walioguswa na kifo hicho.
Mhe.
Rais Magufuli amesema alifanya kazi na Marehemu Philemon Ndesamburo wakati wote
wakiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wote
walishirikiana, kutaniana na anamkumbuka kwa namna ambavyo alitumia muda wake
bungeni kupigania mambo yenye maslai kwa wananchi wa jimbo lake la Moshi Mjini.
Mhe.
Dkt. Magufuli ameitaka familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo na wote
waliguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu na amemuombea
Marehemu apumzishwe mahali pema peponi, Amina.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment