MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Utangazaji (TBC),
Dk. Ayoub Rioba amesema chaneli ya utalii itakayokuwa ikirushwa na televisheni
hiyo itazinduliwa Desemba 30, mwaka huu.
Amesema chaneli hiyo itasaidia kukuza sekta ya
utalii nchini kwa kuwa kila Mtanzania pamoja na wageni wengine wataweza
kufahamu sekta ya utalii ya Tanzania kupitia chaneli hiyo.
"Tunatarajia kumaliza andiko Agosti 10
ambalo litaenda sambasamba na uombaji wa leseni ambao tunatarajia itakuwa
Septemba 10," amesema Dk Rioba wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa
wahariri na wanahabari waandamizi wa masuala ya utalii unaofanyika mkoabi Tanga.
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah akifuatilia mkutano huo unaoendelea na mkoani Tanga Waandishi mbalimbali wa habari nchini wakisikilza mada wakati wa mkutano wa Hifadhi za Taifa, Wahariri na Waandishi wa habari waandamizi nchini unaofanyika jijini Tanga.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment