RAIS Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
kumsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Grace Hokororo (pichani)asimamishwe
kazi kwa tuhuma za kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya
kuishi kinyume cha taratibu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji.
Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali uraia
nchini.
Amesema haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na
wanapewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.
“Idara ya
Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia
bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu Wasomali
kuingia bila kufuata taratibu.”
Waziri Mkuu amesema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini “Tulidhani
ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa Wasomali hao ambao hawakuwepo nchini
wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu sasa hii ni dosari
hatuwezi kuivumilia.”
Amesema Serikali inaitegemea Idara ya Uhamiaji kwa kuzuia mianya
ya uingiaji raia mbalimbali kutoka nje ya nchi bila ya kufuata taratibu, hivyo
Rais Dkt. Magufuli ameagiza Ofisa huyo asimamishwe kazi na uchunguzi ufanyike
ili kubaini malengo yake.
"Hawa Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa
wanaishi nchini wameingia tu na kupewa vibali, hivyo Rais Dkt. John
Magufuli ameagiza ofisa huyo akae pembeni na achunguzwe ni kujua ni kitu gani
kilimsukuma kutoa vibali kwa raia hao."
Pia Waziri Mkuu ameiagiza idara ya Uhamiaji wadhibiti kitengo
cha utoaji hati za kusafiria za Kibalozi na kwa wanaomaliza muda wasipewe tena.
" Lazima hati hizo zikaguliwe katika mipaka yote na maeneo yote ya usafiri
ili kujua kama huyo anayeitumia bado anahadhi hiyo na msiporidhika ichukuweni
kwani kuna watu wanazitumia vibaya."
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment