Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday 28 January 2017

SERIKALI KUTUMBUA WAHUJUMU WA TAZARA

Meneja wa Karakana ya Dar es Salaaam ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Eng. Timothy Kayani, akimwonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa vipuri vya treni vilivyotengenezwa katika karakana hiyo jijini Dar es Salaam, alipotembelea karakana ya Mamlaka hiyo kuona utendaji wake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), alipotembelea mamlaka hiyo kuona utendaji kazi.
 ************************
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa  Makame  Mbarawa  amesema Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote ambaye ataendelea kuisababishia hasara Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kwa kuendelea kuihujumu na kusababisha mamlaka kujiendesha kwa hasara.

Profesa Mbarawa ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Tazara, kuangalia utendaji ambapo amebaini matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa na Serikali na kuahidi kuchukua hatua stahiki.

“Ninafahamu kuna watu 10 hapa ambao wao ni chanzo kikubwa cha matumizi mabaya ya fedha na miongoni mwao wapo Watanzania na Wazambia, nawahakikishia kuwa kila atakayetumia vibaya fedha zinazotolewa na Serikali hatutamvumilia kwenye Serikali hii’, amesema Prof. Mbarawa.

Profesa Mbarawa amesema kumekuwa na idadi kubwa ya watumishi ambao hawana tija  na kuagiza menejimenti ifanye uhakiki na kubaini mahitaji halisi ya Watumishi na watakaobainika kuzidi wahamishiwe ofisi ya tazara Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha Prof. Mbarawa ameuagiza uongozi wa Tazara Makao Makuu kuacha mara moja kutumia mtandao ya kampuni binafsi kutuma taarifa za Ofisi na kuagiza kuanza kutumia mtandao wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) mara moja.

‘Nikirudi tena hapa sitaki kuona mnatumia mitandao wa Kampuni binafsi kutuma taarifa za kiofisi ninawaomba muhakikishe mnatumia  mtandao wa TTCL’ amesisitiza Prof. Mbarawa.
 
Kwa upande Meneja wa TAZARA Mkoa wa Tanzania, Bw. Fuad Abdalla amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa mkoa umejipanga vizuri kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa na Mamlaka inajiendesha kibiashara.

‘Kama mkoa tumekuja na mikakati mizuri ya kutumia mifumo ya Tehama kama njia ya  udhibiti wa mapato, kama ulivyona hivi sasa tunakamilisha mfumo wa Tehama tunaoutumia kufatilia treni kila inapoondoka kwenye Stesheni ya Makao Makuu Dar es Salaam na mfumo huu ukikamilika tutawaashawishi na wenzetu wa Zambia kutumia mfumo huu ili tuweze kudhibiti upotevu wa mapato’ Amesisitiza Bw. Fuad Abdalla.

Bw. Fuad ameongeza kuwa pamoja na mifumo mipya ya Tehama Tazara inaendeleza kwa kasi ukarabati wa mabehewa ya abiria na mizigo ili kuongeza tija na kuiwezesha Mamlaka kupata faida.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment