Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Friday 27 January 2017

UHAMIAJI WATAKIWA KUCHUNGUZA KAYA 180 ZILIZOINGIZWA KATIKA MPANGO WA TASAF WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI WILAYANI KAKONKO

 MKUU  wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma, Kanal Hosea Ndagala akizungumza na mmoja wa wananchi katika vijiji vya Kata ya Nyabibuye alipotembelea.
MKUU  wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma, Kanal Hosea Ndagala ameitaka Idara ya Uhamiaji kuharakisha kufanyia  Uchunguzi kwa  kaya 180 ambazo zilizobainika kuwa na wakuuu wa kaya ambao walidhaniwa ni wahamiaji haramu walioingizwa kwenye mpango wa kusaidia kaya maskini TASAF kinyume cha sheria.
 
Kanali Ndagala aliwataka Wanufaika na walengwa wa TASAF Kutumia fedha wanazo zipata kuanzisha miradi midogomidogo itakayo wasaidia kutoka katika wimbi kubwa la umasikini, na kuacha kutumia fedha hizo kinyume na utaratibu  uliokusudiwa kwa kufanyia mambo ya anasa.

Kauli hiyo aliitolewa jana wakati wa ziara yake vijijini ya kutembelea wanufaika wa Mradi huo katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga ambapo alisema lengo la serikali kuanzisha Mfuko huo ni kusaidia Wataanzania wanaoishi katika Mazingira magumu waweze kupata fedha za kuwapeleka Shule watoto, kupata chakula milo mitatu kwa siku na kuboresha afya zao na kuanzisha miradi itakayo wasaidia kujikwamua na umasikini.

Alisema katika uhakiki uliofanyika wa kuhakiki watu wasio stahili kuwemo katika mradi huo iligundulika kwa Wilaya ya Kakonko kuna baadhi ya kaya 180 zinazo nufaika na mradi huo ambapo baadhi ya wakuu wa kaya hizo mmoja wao ni Raia kutoka Nchi ya Burundi wanao endelea kunufaika na mradi kinyume na utaratibu uliowekwa kwa Wanufaika wa Mradi huo.

Ndagala alisema  kuwahudumia wahamiaji haramu kwenye mpango wa TASAF ni kuhujumu uchumi wa serikali , endapo itagundulika Watu hao tunao wadhania sio raia ikithibitisha na Maafisa wa Uhamiaji Watatakiwa kurudisha fedha zote walizo kwisha kuzichukua na kwa Wale wajumbe wa Kijiji walio shiriki kupitisha majina yao yaingizwe kwenye mradi watatakiwa  kuchukuliwa hatua .

"Leo nimepita mimi mwenyewe kujionea Wanufaika wa Mradi wa TASAF na nimebaini mambo machache moja wapo ikiwa  wahamiaji haramu kuingizwa kwenye mpango, Wanufaika kutumia fedha kama inavyo takiwa wengi wao wanarumia kunywea pombe na mambo mengine nimekuja kuwahamasisha watumie fedha hizo kwa kuwajenga kiuchumi na kwa wale walio bainika kwenye uhakiki  majina tumeyafikisha kwa idara ya uhamiaji waweze kufanya upembuzi yakinifu ilikuweza kubaini uraia wao",alisema Kanali Ndagala.

Sauda Lumala ni Mmoja kati ya Wanufaika alisema kwa upande wake alipo pokea fedha za TASAF alinunua Mbuzi na bata ambapo Mpaka sasa anajumla ya Mbuzi  watatu na bata kumi alizo zalisha kupitia miradi ya kusaidia Kaya masikini.

Alisema changamoto wanayo kumbana nayo katika suala zima la kuanzisha miradi baadhi ya Wanawake wengi wakipokea fedha hizo waume zao wanawanyang'anya na kuzifanyia mambo yao binafsi hali inayopelekea kushindwa kutumia fedha hizo kwa shughuli zilizo kusudiwa.

Nae Mratibu wa TASAF Wilaya ya Kakonko, Maria Tarimo  alisema mpaka sasa kuna jumla ya wanufaika 7775 katika wilaya ya Kakonko zinanufaika na mpango huo ambao umeleta manufaa makubwa na wengi wao wameanza kufikia malengo yaliyopangwa na wameanzisha miradi endelevu itakayo wasaidia kupambana na umasikini.
 
Alisema katika uhakiki wa Kuwaondoa watu wasio stahili katika Mpango huo waliobainika ni  watu 180 wanaozaniwa kuwa sio Raia ambao wataondolewa kwenye mpango huo na watatakiwa kurudisha fedha walizo kwisha kuzichukua kinyume na utaratibu.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment