Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 20 June 2017

NGULI WA TIMU ZA TAIFA ZA WANAWAKE DUNIANI KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI KATIKA KRETA YA MLIMA KILIMANJARO.

Baadhi ya wapagazi Zaidi ya 300 wakijiandaa kwa ajili ya safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro katika Lango la Lemosho kusindikiza ugeni wa kund la wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa kutoka mataifa mbalimbali nchini .
Wachezaji wa timu za taifa kutoka mataifa mbalimbali nchini ,wakishuka katika gari mara baada ya kuwasili katika lango la Lemosho kwa ajili ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuweka historia ya kucheza mchezo a kirafiki eneo la Kreta katika kilele cha Uhuru.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ,Twiga Stras ambaye kwa sasa anakipiga timu ya IFA Academy ya nchini Dubai,Rajvi Ladha akifurahia jambo na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Tengeneza.
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania ,Twiga Stars ,Rajvi Ladha akiandika jambo muda mfupi baada ya kuzungumza na wanahabari juu ya mchezo huo ,
Wachezaji wa timu za Volcano fc na Gracier fc wakikamilisha taratibu kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya mchezo wa kirafiki utakao pigwa June 26 mwaka huu katika kilele cha Uhuru.
Afisa Uhusiano Mkuu wa TTB ,Geofrey Tengeneza akipata taswira ya pamoja na wachezaji hao.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini,TTB Geofrey Tengeneza akieleza jambo kwa wachezaji hao muda mfupi kabla ya kuanza safafri ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mwakilishi wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Willy Lyimo akizungumza na wachezaji hao kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya wachezaji wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza safari ya kupanda Mlima Kilimanjao.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment