Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza.
Serikali ya Tanzania inafanya maboresho ya Mfumo wa
Usajili uliopo na kuanzisha mfumo utakaofanya kazi vizuri usajili wa
matukio muhimu ya binadamu na takwimu nchini unaofanywa na Wakala wa
Usajili, Ufilisi na Udhamini - RITA
Waziri wa
Katiba na Sheria Prof. Palamagamba KABUDI amesema hayo mjini Dodoma
wakati akifungua mkutano wa wadau wanaojadili mfumo huo.
Amesema
maboresho ya mfumo huo yanatekelezwa kupitia Mkakati wa Kitaifa wa
usajili wa Matukio muhimu ya binadamu na takwimu (Civil Registration and
Vital Statistics(CRVS).
Prof Kabudi amesema Mfumo
huo unalenga kutatua changamoto mbalimbali ambazo zimefanya hali ya
usajili wa Matukio muhimu ya binadamu kutokuwa ya kuridhisha nchini.
Ameongeza
kuwa ana imani kuwa utekelezaji wa mkakati huo itakuwa njia sahihi
itakayowezesha kumuona kila mwananchi katika picha ya taifa.
Mkutano huo wa wadau wa usajili wa Matukio muhimu ya mwanadamu nchini umeandaliwa na RITA
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment