Kocha mkuu wa timu ya soka ya Rukwa Lusekelo Sued amelaumu maandalizi yaliofanywa na timu yake kwajili ya mashindano ya Umoja wa michezo wa shule ya msingi nchini (UMITASHUMTA)iliyoanza jana katika viwanja vya shule ya msingi Butimba.
Akizungumza na gazeti hili baada ya kipigo cha bao 1-0 kutoka Katavi,Sued alisema ilichogharimu timu yao ni maandalizi ya zima moto.
"Kiukweli hatukuwa na muda wa kutosha kwajili ya mashindano haya tulijiandaa kwa siku nne kisha tukaja huku"Sued alisema.
"Kiukweli hatukuwa na muda wa kutosha kwajili ya mashindano haya tulijiandaa kwa siku nne kisha tukaja huku"Sued alisema.
Sued amewaomba wadau wa soka nchini wahakikishe wanashirikiana na mikoa mbali mbali katika maandalizi ya kuandaa timu zao za soka.
Mkoa wa Rukwa upo Kundi A pamoja na timu za Iringa,Tabora, Pwani na Katavi.
Katika kundi A inatakiwa zipite timu mbili tu huku kundi B ,C,D,E na F inatakiwa kupita timu moja tu.katika mechi nyingine soka wavulana Iringa iliipoteza kwa mabao 4-2 dhidi ya Tabora na Mara 4-0 Singida.
Katika mchezo wa mpira wa Kengele (Goal Ball), timu za wavulana Kilmanjaro ilianza vyema baada ya Kushinda mabao 8-3 dhidi ya Kagera.Dar-es-salaam iliifunga Shinyanga mabao 13-5.
Timu ya Kilmanjaro iliwakilishwa na God love,Casmiry Josia huku Kagera iliundwa na wachezaji Elias Jackson,Innocent Renatus na Coronel Chrizistom.
Mratibu mkuu wa michezo,ofisi ya Rais Tamisemi,Salum Mkuya alisema mashindano yako njema na kuna vipaji vya hali ya huu.Mkuya amewaomba wadauKatika mbali wajitokeze kwa wingi katika kuchagua wachezaji watakaoweza kuwasaidia kwa miaka ya badae
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment