Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19
Januari, 2017 amewateua Mabalozi watano kuiwakilisha Tanzania katika nchi
mbalimbali.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja Mabalozi
walioteuliwa na vituo vyao vya kazi kama ifuatavyo;
- Balozi Mbelwa Brighton Kairuki ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Beijing – China.
- Balozi George Kahema Madafa ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Rome – Italy.
- Balozi Emmanuel John Nchimbi ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Brasilia – Brazil.
- Balozi Fatma M. Rajab ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Doha- Qatar.
- Balozi Prof. Elizabeth Kiondo ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Ankara – Uturuki.
- Balozi Dkt. James Alex Msekela ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Geneva – Umoja wa Mataifa.
Mabalozi hawa
wataapishwa kesho tarehe 20 Januari, 2017 saa 10:30 Jioni Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua
Bw. Muhidin Ally Mboweto kuwa Balozi.
Tarehe ya
kuapishwa na kituo cha kazi cha Bw. Muhidin Ally Mboweto kitatangazwa baadaye.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment