Na Mwandishi wetu, Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo amesema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua wawekezaji
wanaochochea migogoro katika wilaya ya Ngorongoro na kusababisha uvunjifu wa
amani hivyo kuchangia kuzorota kwa shughuli za maendeleo.
Gambo ameyasema hayo katika
ziara yake wilayani Ngorongoro inayolenga kutatua migogoro wa pori tengefu
lenye ukumbwa wa kilomita za mraba elfu kumi na tano ambapo amekutana na wadau
mbalimbali ikiwemo wawekezaji,wafugaji pamoja na viongozi wa kiserikali.
Amesema kuwa serikali
itawaondoa wawekezaji wanaochochea migogoro na kuwagombanisha wananchi na
serikali yao jambo ambalo halitafumbiwa macho
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro
Rashid Taka amesema kuwa wako baadhi ya watu wanaonufaika na migogoro hiyo
hivyo kumalizika kwa migogoro hiyo kutaleta manufaa kwa wananchi wengi
kuliko kunufaisha kundi la watu wachache
Kwa upande wake Naibu Waziri
wa Wizara ya Mifugo,Kilimo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Ngorongoro
Wiliam Ole Nasha na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Lekule Laizer wamesema kuwa utatuzi wa mgogoro huo
utasaidia kuepusha migongano ya kimaslahi na kuchochea shughuli za
kimaendeleo badala ya kutumia muda mwingi katika usuluhishi wa miigogoro hiyo
Mkuu wa Mkoa ameanza Ziara
yake leo Wilayani Ngorongo na kesho atatembelea katika vijiji mbalimbali ikiwa
ni katika juhudi za kutatua mgogoro wa pori tengefu katika wilaya hiyo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment