Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Khamisi Kigwangalla akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Walemavu wa Afya ya Akili (TUSPO), waliomtembelea Bungeni jana Mei 22.2017, Bungeni mjini Dodoma.
Wabunge wa Viti Malum, Amina Mollel (kushoto) na Stellah Ikupa wakiwa katika kikao hicho na Naibu Waziri.
*****************
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mh. Dkt. Khamisi Kigwangalla amekutana na viongozi wa Chama Cha
Walemavu wa Afya ya Akili (TUSPO), waliomtembelea Bungeni jana Mei
22.2017, Bungeni Dodoma.
Viongozi
hao walikaribishwa na Wabunge wawakilishi wa Watu wenye changamoto
mbali mbali za ulemavu nchini, Mhe. Amina Mollel (Mb.) na Mhe. Stella
Ikupa (Mb.).
Katika kikao hicho Dkt. Kigwangalla ameweza kujadiliana nao
mambo mbalimbali viongozi hao wa TUSPO ikiwemo uanzishwaji wa Kliniki
ya Afya ya Akili kupitia Hospitali zote za Rufaa za Mkoa hapa nchini.
“Nimekutana
na Viongozi wa TUSPO ambao wanashughulika na masuala ya Afya ya Akili.
Tulijadili mambo mengi na niliwaelezea mikakati mbalimbali
inayotekelezwa na Serikali kwenye eneo hili, ikiwemo Uanzishwaji wa
Kliniki za Afya ya Akili kwenye Hospitali zote za Rufaa za Mkoa nchini
nzima. Lakini pia Uanzishwaji wa Rehabilitation Centers kwenye kila
kanda na usambazaji wa Madaktari bingwa wa Afya ya Akili na wataalamu
wote wanaohitajika kutoa huduma hizi kwenye Hospitali na vituo hivi”
Ameeleza Dkt. Kigwangalla.
Aidha,
ameongeza kuwa, amewaahidi uongozi huo wa TUSPO, kuwa atafuatilia juu
ya hatua ambayo mchakato wa kukamilisha muundo wa kisheria (legal
framework) ulipofikia na sababu za kukwama kwake toka sheria ya afya ya
akili ilipotungwa mwaka 2008.
“Serikali
ya awamu ya tano ni sikivu kwa wananchi wake bila kubagua. Nina aahidi
kulifuatilia sualala uanzishwaji wa Baraza la Afya ya Akili, kwani
tayari sheria ilishatungwa muda mrefu.
Na kwamba ni kwa nini Baraza la
Afya ya akili halijaanzishwa toka sheria itungwe mpaka leo na kwa nini
mpaka leo hakujawa na kanuni za Afya ya akili kuelekeza juu ya mambo
mbalimbali” alieleza Dkt. Kigwangalla ambapo amewaahidi kuwapa taarifa
ya utekelezaji wa masuala hayo kwenye Bunge la Mwezi
Kuhusu Magonjwa ya Akili:
Magonjwa
ya akili ni magonjwa ambayo yanaathiri uwezo wa mtu kufikiri, kuhisi,
kutambua na kutenda, na hivyo kuwa na tabia au mwenendo uliotofauti au
usioendana na jamii husika kiimani, kimila, desturi, na nyanja nyingine
za kijamii.
Tabia hizo zinatokana na ugonjwa wa akili kuathiri ufanisi
na shughuli za mtu husika (mgonjwa) au huathiri jamii nzima
inayomzunguka endapo mgonjwa huyo hatopatiwa matibabu stahiki na kwa
wakati muafaka.
Kwa
Tanzania imeeelezwa kuwa baadhi ya wagonjwa wengi wa akili hawafiki
katika vituo vya kutolea huduma za afya na badala yake kuishia kwenye
tiba za jadi au kutelekezwa na kunyanyapaliwa huku takwimu za
zinaonyesha kuwa Tanzania ina idadi ya watu takriban milioni 45 na
kutokana na taarifa ya afya ya akili kwa mwaka 2014/15 inaonyesha kuwa
idadi ya watu 817,532 wanaugua magonjwa mbalimbali ya akili nchini, hii
ni karibu asilimia 2 ya watanzania wote.
Pia
idadi hii ni ongezeko la wagonjwa 367,532 ukilinganisha na takwimu za
mwaka 2013/14 walikuwa ni 450,000. Kati ya wagonjwa wote wa akili kwa
mwaka 2014/15 wanawake ni ni 332,000 na wanaume ni 485,532.
Mkoa
wa Dar-Es-Salaam unaongoza kwa kuwa n awagonjwa wengi nchini ukifuatiwa
na mkoa wa Dodoma na mkoa wa mwisho ni Lindi. Idadi hiyo ya wagonjwa ni
wale walioweza kuhudhuria katika vituo vya kutolea huduma ya afya hapa
nchini.
Sheria ya afya ya akili imeundwa mwaka 2008. Miaka tisa hadi sasa hakuna kanuni za utekelezeji wa sheria hiyo!!
ReplyDelete