Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli
akisalimiana na Mwenyekiti wa tasisi ya Bill and Melinda Gates
Foundation , Bill Gates aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye
Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli
akizungumza na Mwenyekiti wa tasisi ya Bill and Melinda Gates
Foundation, Bill Gates aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo
Agosti 10, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli
akiagana na Mwenyekiti wa tasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation,Bill Gates aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini
Dar es salaam leo Agosti 10, 2017. Pamoja nao ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles
Tizeba (wa tatu Kushoto), Msaidizi wa rais Masuala ya diplomasia ,
Zuhura Bundala (kushoto) pamoja na maafisa alioongozana nao, Bill
Gates.
*******************
Taasisi
ya Bill and Mellinda Gates imetenga Dola za Marekani Milioni 350 sawa na
takribani Shilingi Bilioni 777.084 za Tanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi
mbalimbali katika sekta ya kilimo, afya na mifumo ya kielektroniki ya
upatikanaji wa taarifa.
Mwenyekiti
Mwenza wa taasisi hiyo, Bill Gates amesema hayo leo tarehe 10 Agosti, 2017
Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Bill Gates amesema kama ambavyo taasisi yake imeshirikiana na Tanzania kwa
kiasi kikubwa katika kuimarisha huduma za afya hapa nchini, fedha hizo zitaelekezwa
katika utekelezaji wa miradi zaidi ya afya ikiwemo kupunguza vifo vya uzazi,
kukabiliana na ugonjwa wa malaria, kuimarisha lishe na kukabiliana na
utapiamlo, zitaelekezwa katika sekta ya kilimo ambako zitasaidia kuongeza
uzalishaji wa mazao, kuzalisha mbegu bora na kuboresha ufugaji utakaoongeza
chakula na pia zitasaidia kuweka mifumo ya kisasa ya upatikanaji wa taarifa.
Bill Gates ameelezea kufurahishwa na maendeleo ya uchumi wa Tanzania pamoja na
uongozi na msimamo wa Rais Magufuli juu ya kutaka miradi hiyo ilete matokeo
yenye manufaa, na amesema atakuja Tanzania mara nyingi ili kuimarisha zaidi
ushirikiano na kufuatilia utekelezaji wa miradi.
Kwa
upande wake, Rais Magufuli amemshukuru,Bill Gates kwa mchango mkubwa
unaotolewa na taasisi ya Bill and Mellinda Gates katika miradi mbalimbali hapa
nchini ikiwemo fedha ambazo taasisi hiyo itazitoa katika kipindi cha miaka
mitano kuanzia sasa na amemhakikishia kuwa Serikali yake itahakikisha fedha
hizo zinaleta matokeo yaliyokusudiwa.
Mazungumzo
kati ya Rais Magufuli na Bill Gates yamehudhuriwa na Waziri wa Kilimo,
Ufugaji na uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto,. Ummy Mwalimu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment