Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni
Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana
na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na
wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi,
Tarafa ya Kibiti. Chini ni silaha 8 aina
ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon
Sirro akionesha makasha ya risasi (magazine)
ambazo ni miongoni mwa makasha 8 yaliyokuwa yakitumiwa na
wahalifu katika eneo la Tangibovu,
Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kushoto ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli
Musa akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni
Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas.
Katika tukio hilo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua wahalifu 13 ambao
walikuwa wakifanya mauaji Kibiti.
Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, IGP Simon Sirro akielezea
baadhi ya vitu mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu 13 waliouawa
katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya
Kibiti ambapo jumla ya silaha 8 aina ya SMG, risasi
158, pikipiki 2, pamoja na begi
la nguo vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu hao. Kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa
ya jinai (CP) Robert Boaz
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro
akionesha silaha aina ya SMG ambayo ni miongoni mwa silaha 8 zilizokuwa zikitumiwa na wahalifu 13 waliouawa
katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni
Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kulia ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa
akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni Maalumu
za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas.
Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, IGP Simon Sirro akiongea na
wananchi wa Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti alipokuwa
akitoka kukagua eneo la tukio walipouawa
wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi katika eneo la Tangibovu. – Picha na Jeshi La
Polisi
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment