Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday, 29 April 2017

WAZIRI KAIRUKI AZINDUA BODI YA KIMA CHA CHINI CHA MASHAHARA

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro(aliyesimama) akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah J. Kairuki (Mb) kuzindua Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Sekta ya Umma kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mapema leo.
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ,  Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Sekta ya Umma kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyofanyika mapema leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Sekta ya Umma,Gertrude Mpaka (katikati) akizungumza baada ya uzinduzi wa bodi hiyo katika  ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mapema leo
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah J. Kairuki (Mb) (wa nne kutoka kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro  (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Sekta ya Umma baada ya kuizindua bodi hiyo mapema leo.


MKUU WA MKOA WA MBEYA AWAONGOZA WAKAZI WA JIJI LA MBEYA KUFANYA USAFI SOKO LA WAMACHINGA NANENANE

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (wapili kushoto) akishiriki kufanya usafi katika Soko jipya la Machinga lililoo nanenae jijini Mbeya leo.
Wananchi wakishiriki kufanya usafi.
Wafanyakazi wa Benki ya Akiba wakiwa na Mkoo wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla baada ya kufanya usafi.
Baadhi ya maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama walioshiriki katika kufanya usafi leo

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewaongoza wakazi wa jiji la Mbeya kufanya usafi katika soko la wamachinga la Nanenane jijini humno leo.

Akizungumza wakati wa kufanya usafi Makalla amewahimiza wakazi wa Mbeya kuunga mkono kampeni ya kuliweka jiji la Mbeya na mkoa na halmashauri zote kuwa safi.

Aidha Makalla ameishukuru Benki ya Akiba kutoa msaada wa Vifaa vya usafi, na wafanyakazi wa Akiba Bank kushiriki kufanya usafi na Benki hiyo kukubali ombi lake  kutoa mikopo kwa wamachinga.

Meneja wa Akiba Tawi la Mbeya Amehaidi kukutana na wamachinga hao na wengine katika masoko maalum kwanza kuwapa Mafunzo na baadaye kuwapatia mikopo.

Mbali na Mkuu wa Mkoa na Wafanyakazi hao wa Benki pia viongozi wa vyama vya Siasa , vyombo vya ulinzi na usalama na wamachinga walijitokeza kufanya usafi katika soko la nanenane ambalo litakalofunguliwa hivi karibuni kwa ajili ya Machinga wapatao 1,500

Wakizungumza katika risala yao wamachinga wamemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwasaidia kujengwa kwa choo cha kisasa , kuwekwa umeme na Maji katika soko hilo na kuahidi kuhamia sokoni hapo ifikapo Julai mosi.

Mkuu wa Mkoa amemwagiza  Mkuu wa usalama barabarani na Sumatra kuweka kituo cha Daladala katika eneo hilo mapema wiki ijayo jambo ambalo wamachinga wamelipongeza kwani litachochea biashara


RAIS DKT MAGUFULI APOKELEWA KWA SHANGWE NA NDEREMO MKOAN KILIMANJARO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongiozana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Rais wa TUCTA Bw. Tumaini Nyamhokwa alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu Mhe. Kassim majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aiiongiozana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wanahabari alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wana UVCCM alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi wa Bomang'ombe Wilaya ya Hai waliomsimamisha kwa muda wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi wa Bomang'ombe Wilaya ya Hai waliomsimamisha kwa muda wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.


SOKO LA MWEMBE TAYARI DODOMA LATEKETEA KWA MOTO

 Wafanya biashara katika soko la wauza vifaa chakavu vya magari na mitambo pamoja na vya ujenzi la Mwembe Tayari mjini Dodoma wakifarijiana baada ya soko hilo kuteketea kwa moto lote usiku wa kuamkia leo.
 Nimajonzi tupu kwa wafanya biashara soko la Mwembe Tayari hasa ukizingatia kua biashara nyingi siku hizi mitaji yake ni mikopo toka taasisi za fedha.
 Wananchi wakiangalia mabaki.
Chanzo cha moto inaamini ni mmoja wa akina mama ntilie ambao hua na tabia ya kubandika maharagwe na kuyaacha yakiendelea kuiva usiku kucha bila uangalizi wowote.
Na Urban Epimark, Dodoma.
SOKO la wauza vifaa chakavu vya magari na mitambo pamoja na vya ujenzi la Mwembe Tayari mjini Dodoma limeshika moto na kuungua lote usiku wa kuamkia leo.

Soko hilo lililopo makutano ya barabara ya kuelekea Singida lenye wafanyabisha mchanganyiko ambao ni wajasiriamali, hua ni mkombozi mkubwa kwa watu tofauti mjini Dodoma.

Naibu Mwenyekiti wa Soko hilo Bw Aloyce Emanuel Mboro, ameeleza idadi ya mabanda yalitoungua ni takribani 80 na yenye mali, ambapo hakuweza kutoa makadirio ya thamani yake.

Nae mhanga aliyeunguliwa banda lake Bw Salvatory Joseph Shio akieleza kwa uchungu kwamba banda lake limeungua lote, na lilikuwa na mali yenye thamani ipatayo millioni 30 na amekopa benki, ana familia na anasomesha watoto, hajui cha kufanya.

Salvatory ameeleza pia chanzo cha moto inaamini ni mmoja wa akina mama ntilie ambao hua na tabia ya kubandika maharagwe na kuyaacha yakiendelea kuiva usiku kucha bila uangalizi wowote.

Inasemekana ni vipande vya cheche za moto, ziliruka na kushika banda moja na kupeperushwa na moto na kuenea kwingine.

Aidha, walinzi wenye kulinda soko hilo ambao wapo nane, wote walikimbia kujificha ili kuhofia hamaki na hasira za wafanyibiashara.

Huduma ya Zimamoto, inavyosemekana walifika sokoni hapo majira ya saa 06:30 usiku, moto ulikuwa mkubwa na hawakuweza kuudhibiti, badala yake walilinda kituo cha mafuta kilichopo jirani ili moto usilete madhara zaidi.

Hakuna afisa yeyote wa serikali aliyeweza kupatikana asubuhi hii wala Diwani wa eneo hilo, bali wahanga wameiomba serikali iwaangalie kwa jicho la huruma ili waweze tena kuyamudu maisha.


MOTO WAACHA MAJONZI SOKO LA WAUZA MBAO KAMBARAGE SHINYANGA

Moto mkali ulio ibuka usiku wa leo katika Soko la wauza mbao la Kambarage mjini Shinyanga limeacha vilio na majonzi kwa wafanya biashara wa soko hilo.

Moto huo ambao chanzo chake bado hakijabainika uliteketeza shehena ku wa ya mbao katika soko hilo na kiasi kidogo tu kiliokolewa. 

Daily NewsHabarileo Blog itakujuza zaidi.


Friday, 28 April 2017

ALICHOKISEMA RAIS MAGUFULI WAKATI AKIPOKEA TAARIFA YA UHAKIKI WA VYETI KWA WATUMISHI WA UMMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia majina hayo pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  mara baada ya kufungua boksi kubwa lenye majina ya watumishi hao wa umma ambao wamegushi vyeti vyao .
Rais Dk John Magufuli akipokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti  kwa Watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.katikati ni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia viongozi mbalimbali, wanafunzi wa UDOM, pamoja na watumishi wa Umma mara baada ya kupokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti  kwa watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.



UKINUNUA MAGAZETI YA DAILY NEWS NA HABARILEO UNAPATA MENGI ZAIDI YA HABARI

 Taarifa za Utabiri wa Hali ya hewa Zipo ndani ya magazeti haya.
Utapapia Msamiati wa Siku wa Neno la Kiswahili.


SASA WAWEZA LIPA KODI ZOTE ZA TRA NA TOZO ZA TPA KUPITIA MATAWI YA TIB CORPARATE BANK



POLISI YAPIGA MARUFUKU WANACHAMA WA CUF KUFANYA USAFI KATIKA MAKAO MAKUU YA CHAMA HICHO

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imezuia wanachama  wa Chama cha Wananchi (CUF) wakiongozwa na Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea kufanya usafi katika ofisi za Makao Makuu ya Chama hichokutokana na kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani.

Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Simon Sirro amesema kutokana na sababu za kiusalama na mgogoro wa muda mrefu unaoendelea ndani ya chama hicho , ni vyema mbunge huyo na wanachama wengine wakafanya usafi katika maeneo yao wanayoishi au kufanyia kazi.

“Kwa kuwa wanaonesha wanapenda kufanya usafi, ningeomba wafanye usafi katika maeneo yao. Tunachokifanya ni kuzuia madhara makubwa yasitokee, hivyo mwana Dar es Salaam yeyote naomba usishiriki katika shughuli hii, kwakuwa kuna dalili makundi haya yakikutana kutakuwa na fujo,” amesema Kamishna Sirro.

Aidha, amesema jeshi hilo linawashikilia watu saba kutokana na vurugu zilizoibuka katika mkutano wa viongozi  wa CUF wilaya ya Kinondoni na wanahabari  ambapo watu mbalimbali walijeruhiwa wakiwemo waandishi wa habari.

Amesema upelelezi umekamilika na jalada limeshafikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa ajili ya kuandaa mashitaka na baadae kufikishwa mahakamani.

Amewataja waliokamatwa kuwa ni pamoja na Ofisa Mahusiano na Mawasiliano wa chama hicho, Abdul Kambaya, mlinzi wa karibu wa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba,  Mtawa Rashid  na Khamis Abdallah maarufu kama Taekwondo.


MIGODI INAYOMILIKIWA NA KAMPUNI YA ACACIA YAWA KIVUTIO KATIKA MAONESHO YA WIKI YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI.

Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya mahala pa kazi yanayofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Maonesho haya yanayohusisha kampuni na Taasisi mbalimbali nchini yanaratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya mahala pa Kazi (OSHA).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,wakiweka sawa moja ya picha inayoonesha eneo ambalo shughuli za uchimbaji unafanyika.
Afisa Uhakiki na Usalama katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA,Amina Mohamed akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,wakitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo katika maeonesho ya wiki ya usalama mahala pa kazi ndani ya viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI


UBA YATOA VYETI KWA WADAU WALIOPATA RUZUKU ZA MRADI

 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akizungumza na wanufaika wa maradi wa kuandika mawazo ya biashara ambao wapo hapa nchini juu ya namna watakvyoweza kushirikiana na Benki ya UBA katika kukuza biashra zao mpaka nje ya mipaka ya Tanzania

 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akikabidhi cheti kwa Hurbert  Mwashiuya juu kama mnufaika wa mradi mara baada ya kupata ruzuku 

 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akikabidhi  cheti kwa Bi , Aika Mtei kma mmoja wa wanufaika wa ruzuku mara baada ya kuandika mradi juu ya biashara katika mtandao
 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akiwaeleza watendaji wa Benki ya UBA juu ya umuhimu wa kuwasaidia wanufaika hao hili waweze kuwa mfano kwa wengine
Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akiwa katika picha ya pamoja na wanufaika na baadhi ya watendaji wa beki hiyo


Thursday, 27 April 2017

RC MAKALLA AUAGIZA UONGOZI WA WILAYA, JIJI, POLISI,SUMATRA, BODABODA, BAJAJI NA DALADALA KUKUTANA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza katika mkutano wake wa kupokea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi kwa utaratibu maalum aliyojiwekea kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Kushoto  ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William Ntinika.
wananchi wakiuliza maswali
Wakazi wa jiji la mbeya waliohudhuria mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akifafanua jambo kwa wanahabari.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amemeuagiza uongozi wa Wilaya, Jiji la Mbeya,Polisi, Sumatrapamoja na viongozi wa Bajaji, Daladala na Bodaboda kukutana na kuboresha namna ya utoajibhuduma ambao utaepusha ajali, msongamano katika jiji hilo.

Makalla amesema lazima jiji la Mbeya liwe safi na liwe la mfano katika kila nyanya ikiwepo ya utoaji huduma ya usafiri kulinganisha na maemeo mengine nchini.

Ameomba ushirikiano kwa viongozi, watendaji na wananchi kuunga Mkono jitihada hizo.

Katika kuhakikisha hilo linafanyiwa kazi haraka, Makalla ameahidi kuitisha mkutano  muda wowote na wenyeviti na makatibu wa Mabaraza ya Ardhi ngazi ya Wilaya kufuatia malalamiko  mengi kuelekezwa kwenye Mabaraza ya ardhi.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa kusikiliza kero za wananchi utaratibu ambao ameuweka tangu alipoteuliwa mwezi machi mwaka jana ambapo Mkuu wa Mkoa husikiliza kero za wananchi mara mbili kwa mwezi.

Utaratibu huu umepongezwa na wananchi na umesaidia sana kutatua kero nyingi za wananchi.