POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imezuia wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wakiongozwa na
Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea kufanya usafi katika ofisi za Makao Makuu ya
Chama hichokutokana na kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani.
Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Simon Sirro amesema kutokana
na sababu za kiusalama na mgogoro wa muda mrefu unaoendelea ndani ya chama
hicho , ni vyema mbunge huyo na wanachama wengine wakafanya usafi katika maeneo
yao wanayoishi au kufanyia kazi.
“Kwa kuwa wanaonesha wanapenda kufanya usafi, ningeomba
wafanye usafi katika maeneo yao. Tunachokifanya ni kuzuia madhara makubwa
yasitokee, hivyo mwana Dar es Salaam yeyote naomba usishiriki katika shughuli
hii, kwakuwa kuna dalili makundi haya yakikutana kutakuwa na fujo,” amesema
Kamishna Sirro.
Aidha, amesema jeshi hilo linawashikilia watu saba kutokana
na vurugu zilizoibuka katika mkutano wa viongozi wa CUF wilaya ya Kinondoni na wanahabari ambapo watu mbalimbali walijeruhiwa wakiwemo
waandishi wa habari.
Amesema upelelezi umekamilika na jalada limeshafikishwa kwa Mkurugenzi
wa Mashitaka (DPP) kwa ajili ya kuandaa mashitaka na baadae kufikishwa
mahakamani.
Amewataja waliokamatwa kuwa ni pamoja na Ofisa Mahusiano na
Mawasiliano wa chama hicho, Abdul Kambaya, mlinzi wa karibu wa Mwenyekiti wa
CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mtawa Rashid
na Khamis Abdallah maarufu kama
Taekwondo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment