Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, 7 March 2018

WANANCHI LINDENI NA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI

 Waziri wa Nishati Dkt. Merdad Kalemani akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau wa  Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau wa  Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa.
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau wa  Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau wa  Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa.
 Waziri wa Nishati dkt. Merdad Kalemani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua wakiteta jambo wakati wa Warsha ya Wadau wa  Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa.
Naibu wa Nishati, Subira Mgalu na Mkuu wa mkoa Iringa Amina Masenza wakiteta jambo wakati wa Warsha ya Wadau wa  Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani (kushoto) Naibu waziri wa Nishati (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza (kulia) wakiwa nje ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa.
washiki wa Warsha ya Wadau wa  Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa.

 Na Zuena Msuya , Iringa
Waziri wa Nishati Dkt.Kalemani amewataka Viongozi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na wadau mbalimbali kuwaelimisha Wananchi juu ya umuhimu wa kutunza na kulinda vyanzo vya maji nchini ili yatumike kuzalisha umeme mwingi na pia katika matumizi bora ya Kilimo cha umwagiliaji.

Dkt.Kalemani alisema hayo wakati wa Warsha ya Wadau wa  Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 inayofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa.

Warsha hiyo ilishirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji ili kupata Elimu kuhusu faida na umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji yanayoingiza maji yake katika bonde la Mto Rufiji patakapojengwa Mradi wa Kuzalisha Umeme wa megawati 2,100 kwa kutumia maporomoko ya maji katika Bonde la  Mto Rufiji.

Katika warsha hiyo, Dkt.Kalemani alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa Mradi mkubwa wa kuzalisha umeme kwa kutumia Maporomoko ya Maji katika bonde la Mto Rufiji, ni vyema Wananchi wakaelimishwa umuhimu wa kutunza maji kwa ajili ya Nishati ya umeme pamoja na matumizi mengine ikiwemo kilimo ili shughuli hizo zitekelezwe kwa pamoja pasipo kutokea athari yoyete.

Aliweka wazi kuwa mbali na Mradi huo kuzalisha umeme, pia eneo hilo litakuwa kivutio kikubwa cha utalii kwa kuwa lipo katika hifadhi ya Taifa ya mbuga ya wanyama ya Selou pamoja hivyo  kungizia Serikali mapato yatokanayo na utalii pamoja na biashara zitazokuwa zikiendeshwa katika eneo hilo.

Vilevile alisema kuwa Wizara zote zitashirikiana kutekeleza Mradi huo kwakuwa utekelezaji wake unahusisha Wizara mbalimbali zikiwemo Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Maliasili na Utalii, pamoja na Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano .

Alieleza zaidi kuwa hadi kufikia kwezi Julai  mwaka huu Mkandarasi atayetekeleza Mradi huo atakuwa amekwishapatikana na kuanza ujenzi wa mradi huo utakaokamilika kwa kipindi cha miaka 3, ambapo pamoja na mambo mengine kinachofanyika Sasa katika eneo la mradi huo ni ukamikishaji wa miundombinu ya Barabara, Reli , Maji pamoja na Umeme vitakavyotumiwa na mkandarasi wakati wa kutekeleza Mradi huo.

Nae Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, alieleza kuwa Mradi huo ni fursa kubwa ya ajira za muda mfupi na zile za muda mrefu kwa watanzania wenye taaluma husika na wale walio na uwezo na ujuzi.

Amewataka watanzania hasa Vijana kuchangamkia fursa hiyo katika kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza aliahidi kutoa elimu kwa Wananchi wa Mkoa wa Iringa ambao sehemu kubwa ya mito yake hutiririsha maji katika Bonde la Mto Rufiji.

Aidha alisema kuwa ataendelea kuwaelimisha Wakazi wa Iringa kuweka njia Bora za kilimo cha umwagiliaji zitakazotumika katika kilimo badala ya ile iliyozoeleka ya kulima  Vinyungu katika vyanzo vya maji na Maeneo Oevu.

Kwa upande wao Wabunge wa Mkoa huo akiwepo Mbunge wa Mafinga mjini, Cosato Chumi  na mbunge wa kilolo Venance Mwamoto walisema kuwa watahakikisha Mradi huo unatekelezwa na hakutakuwa na changamoto zitakazoweza kuukwamisha Mradi huo kuanzia hatua za awali Hadi mwisho.

Walisema kwa kutumia nafasi zao watawashirikisha Wabunge wenzao kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa Mradi huo wenye manufaaa makubwa kwa Wananchi na Taifa kwa jumla.


RAIS MAGUFULI AOMBOLEZA KIFO CHA DK KABOUROU



“Kwa masikitiko nimepokea taarifa ya kifo cha Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma Dkt. Walid Amani Kabourou kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 07 Machi, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Dkt. Walid Amani Kabourou atakumbukwa kwa mchango wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM, na alipokuwa Mbunge wa Kigoma Mjini na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Natoa pole kwa familia yake, wana CCM wote, wananchi wa Kigoma, ndugu jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu”

Hii ni sehemu ya salamu za rambirambi alizotuma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga kufuatia kifo cha Dkt. Walid Amani Kabourou.

Pamoja na salamu hizo, Rais Magufuli ameiombea familia ya Marehemu na wote walioguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi na amemuombea Marehemu apumzike mahali pema peponi, Amina.


WCF YAAGIZWA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WAAJIRI 6,907


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(katikati), akizu nguzma jambo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kubaini waajiri ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), jijini Dar es Salaam Machi 6, 2018. Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bi. Rehema Kabongo.
Mhe. Mavunde, na Bi. Rehema wakipitia nyaraka

Raia wa kigeni waliojuwa wafanyakazi wa kiwanda cha kugandisha barafu, wakiwa kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa kosa la kufanya kazi nchini bila kibali.

Raia wa kigeni waliojuwa wafanyakazi wa kiwanda cha kugandisha barafu, wakiwa kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa kosa la kufanya kazi nchini bila kibali.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Bi. Laura Kunenge, (kushoto), akizungumza jambo na Kamishna wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Bi.Hilda Kabisama.

Afisa Mwajiri kiwanda cha Carmel Concrete cha Mbagala Kizuiani akijieleza kwa Naibu Waziri Mavunde baada ya kubainika kiwanda hicho kinakiuka Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini. kwa kutowalinda wafanyakazi kwa kuwapatia vifaa vya kujihami.Kiwanda hicho kimetozwa faini ya zaidi ya shilingi Milioni 10 kwa kosa hilo na mengineyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughhulikia Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde, (mwenye suti), akizunhumza jambo wakati alifanya ziara ya kushtukiza kwenye kiwanda cha Carmel Concrete cha Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam jana (Machi 6, 2018), ili kubaini waajiri ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), na ambao hawatekelezi Sheria ya ajira na mahusiano kazini. Jumla ya waajiri 6,907 jijini Dar es Salaam, hawajajisajili na Mfuko na watapelekwa mahakamani.

Mfanyakazi wa kiwanda cha Carmel akilalamika mbele ya Naibu Waziri Mavunde, kuhusu mazingira mabovu ya kufanyia kazi na mishahara midogo kinyume na maelekezo ya serikali






Naibu Waziri akiumuuliza mfanyakazi huyo wa kiwanda cha kugandisha barafu, ambacho pia kimebainika kufanya shughuli za kuchomelea vyuma, baada ya kumkuta hana viatu vigumu (gumboots)

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughhulikia Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde, akizunguzma mbele ya Meneja wa kiwanda cha Carmel Concrete, Nabil Kassim, (kushoto), kuhusu kutowalinda wafanyakazi wake.

Naibu Waziri akiongozana na Kmaishana wa Kazi, Bi.Hilda Kabisa na maafisa wengine wakati wakiwasili kiwanda cha kugandisha barafu cha Bhogal, huko Mbagala Chamazi nje kidogo ya jiji.
*********************
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
SERIKALI imesema haitabadili msimamo wake wa kuwapeleka mahakamani waajiri wote ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amewaambia waandishi wa habari leo Machi 6, 2018 jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri ametoa tamko hilo wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekelkeza takwa hilo la Kisheria ikiwa ni pamoja na wale ambao hawateketekelezi inavyopasa Sheria ya ajira na mahusiano kazini.

Akiwa kwenye kiwanda cha kugandisha barafu cha Boghal kilichoko Chamazi, Naibu Waziri pia aliahgiza kukamatwa mara moja wafanyakazi watatu raia wa kigeni ambao walikutwa hawana vibali vya kufanyia kazi.

“Dar es Salaam kuna jumla ya waajiri 14,484, na kati ya hao, 6,907, tumebaini bado hawajajisajili na nimewaagiza maafisa wa WCF kuwafikisha mahakamani mara moja kuanzia kesho mashtaka dhidi yao yaandaliwe, (leo).” Aliagiza Naibu Waziri Mavudne ambaye alifuatana na Kamaishna wa Kazi Bi. Hilda Kabisa, na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo.

Aidha Naibu Waziri Mavunde, aliagiza wafanyakazi watatu wa kiwanda cha kugandisha barafu cha Bhogal, kilichoko Chamazi nje kidogo ya jiji kukamatwa na polisi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa kutokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.

“Nitoe wito kwa waajiri nchini, kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha uratibu ajira za wageni, kinaelekeza kuwa hataruhusiwa mgeni yoyote kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali, na hawa tumewauliza vibali vyao hawakuwa navyo kwa hivyo nimeagiza wakamatwe na wapelekwe polisi na kasha wafikishe mahakamani.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Mavunde.

Ziara ya naibu waziri ni muendelezo wa operesheni inayoendelea nchini kote kuwabaini waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kuwabaini wale ambao hawatekelezi Sheria ya ajira na mahusiano kazini.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bi. Rehema Kabongo, alisema Mfuko umeanza kutekeleza maagizo ya serikali kwa kuwafikisha mahakamani wale wote ambao bado hawajajisajili na Mfuko ambao wanakabiliwa na adhabu ya kulipa faini isiyopungua shuklingi Milioni 50, (Milioni Hamsini) au kifungo cha miaka mitano jela au vyote kwa pamoja.

“Nitoe wito kwa wafanyakazi, operesheni hii ndio imeanza na kama bado kuna mwajiri ambaye bado hajatekeleza wajibu wake asisubiri kufikishwa mahakamani.” Alisema.


Monday, 5 March 2018

PROFESA MUBOFU MAKAMU MKUU WA CHUO MPYA UDOM

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Rais Mstaafu (Awamu ya Tatu), Mhe. Benjamin William Mkapa ametangaza uteuzi wa Profesa Egid Beatus Mubofu kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Profesa Idris Suleiman Kikula.

Uteuzi huo umetangazwa rasmi leo tarehe 5, Machi 2018 kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisi ya Mkuu wa UDOM, Mhe. Benjamin Mkapa.

Kabla ya uteuzi huo Profesa Mubofu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), na kabla ya hapo alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa Profesa Mubofu unaanza rasmi tarehe 17 Machi, 2018.

Profesa Idris Kikula ni miongoni mwa wanazuoni waandamizi wanaoheshimika ndani na nje ya nchi kitaaluma kwa kushiriki katika tafiti mbalimbali za kisayansi na kijamii

Ameshiriki katika tafiti hizo kwa kushirikiana na taasisi nguli za kitafiti hapa nchini kama REPOA, pamoja na taasisi ya UONGOZI. UDOM ndio chuo kikuu pekee chenye uwezo mkubwa wa kuchukua wanafunzi wengi hapa nchini na Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na inakadiriwa kina uwezo wa kuchukua wanafunzi takriban 40,000, pia kina eneo la ukubwa wa hekari zaidi ya 6000.


Sunday, 4 March 2018

NAIBU SPIKA TULIA ATOA MSAADA TAASISI ZA DINI MBEYA

 NAIBU Spika Dk.Tulia Ackson ameshiriki ibada takatifu katika kanisa la Jerusalem Temple Sokomatola, Mjini Mbeya ambapo pamoja na kushiriki na waumini wenzake katika ibada hiyo Dk Tulia pia alitoa jumla ya shilingi milioni mbili na laki tano kama msaada wake ikiwa Milioni moja kwa  ajili ya sikukuu ya wakinamama, Milioni moja na nusu alinunua CD mbili za kwaya katika kanisa hilo.
Dk. Tulia akifanyiwa maombi maalum.
Pia Dk Tulia alipata fursa ya kushiriki kama mgeni rasmi kwenye  Maulid ya wanawake wa kiislam mkoa wa Mbeya iliyofanyika katika msikiti wa Masjid Fyii Sabili Ilah uliopo Forest ambapo alitoa msaada wa vitabu vya mafundisho ya kiislam na Quran tukufu pamoja na kulipia huduma zote ikiwemo chakula.
"Sisi kama viongozi yawezekana wakati mwingine tukawa hatuwafikii kwa wakati watumishi wa dini lakini mara zote tupo pamoja nanyi na tunatambua sana mchango wenu katika taifa kwa maombi yenu na haswa katika kuwalewa watoto wetu katika maadili mema ambayo yatasaidia kuwa na raia wazuri wenye kumcha Mungu," Dk Tulia.


Friday, 2 March 2018

WASICHANA WAWILI RAIA WA RWANDA WAKAMATWA NCHINI


SERIKALI YAOMBA USHIRIKIANO ZAIDI NA BENKI YA DUNIA ILI KUHARAKISHA MAENDELEO YA NCHI

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bi. Bella Bird na Mkurugenzi wa Uchumi, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Felipe Jaramilo, mara baada ya kikao kilichofanyika Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uchumi Jumla, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Felipe Jaramilo akifafanua jambo katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza na ujumbe wa Mkurugenzi wa Uchumi jumla, Biashara na Uwekezaji (hawapo pichani), katika kikao kilichofanyika Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 **********************
Na Benny Mwaipaja, WFM
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Dkt. Felipe Jaramilo katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Waziri wa Fedha na Mipango aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuisaidia Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Joseph Magufuli katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maedeleo hapa nchini.

Dkt. Mpango ameeleza kuwa uchumi wa nchi umeendelea kukua kwa kiwango cha kati ya asilimia 6-7 kwa muda na hivyo kuiwezesha Serikali kuendelea na utoaji wa huduma za jamii na kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Dkt. Mpango ameeleza kuwa pomaja na nia ya kuendeleza mafanikio mazuri yaliyopatikana katika awamu za Serikali zilizopita, Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kwa dhati kujenga uchumi imara kwa kuendeleza viwanda na kuweka mazingira mazuri ya biashara ili kuvutia wawekezaji wa ndani na wale wa nje kuja kuwekeza nchini , kujenga miundombinu ya barabara, reli, umeme , viwanja vya ndege na kuongeza uwekezaji katika utoaji wa huduma za jamii kama vile elimu, afya na maji.

Aidha, ameeleza kuwa katika kufikia malengo hayo , Serikali imefanya juhudi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato, kusimamia vizuri matumizi ya fedha za Serikali, kuongeza bajeti ya maendeleo hadi kufikia asilimia kati ya 35 na 40 ya bajeti nzimat, kuongeza ufanisi katika utendaji wa umma na kupambana na rushwa pamoja na mambo mengine.

Pamoja na ukuaji mzuri wa uchumi, Dkt. Mpango alisema kuwa Taifa bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana, kiwango cha umasikini bado kiko juu, ukuaji mdogo wa Sekta ya kilimo ambayo imeajiri takribani asilimia 70 ya watanzania unaosababishwa na ukosefu wa mbegu bora, miundombinu ya umwagiliaji na soko la uhakika, na kupungua kwa mikopo ya benki za biashara kwa sekta binafsi pamoja na mambo mengine.

Katika kusaidi juhudi za Serikali kupambana na changamoto mbalimbali , Dk. Mpango aliiomba Benki ya Dunia kupitia kwa Dk. Felipe kuisadia Serikali mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 150 kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa uchumi na utoaji huduma ( Growth and Service Delivery) amabao uko katika hatua ya maandalizi.

Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Dkt. Felipe Jaramilo, kwa upande wake aliipongeza Serikali ya awamu ya tano ya Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi nzuri inayofanya ya kusimamia uchumi mpana, kuongeza makusanyo ya ndani ambayo yanasaidia upatikana fedha kwa ajili ya kugharamia uwekezaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo, kupambana na rushwa, kusimamia matumizi ya fedha za umma, na kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi za umma.

Aidha, Dkt. Felipe aliishauri Serikali kuwekeza zaidi katika rasilimali watu na miundombinu ili kulifanya Taifa kuweza kuhimili ushindani wa kimataifa dunia na kujenga uchumi unaokua na endelevu.

Vile vile aliieleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita uwekezaji kutoka nje umekuwa zaidi katika Sekta ya madini, hivyo alishauri Serikali kuweka mazingira mazuri ya biashara ili kuwavutia wawekezaji kutoka nje kuwekeza katika sekta za viwanda na utoaji huduma ili kuongeza wigo wa shughuli za kiuchumi na kuchochea ukuaji wake.


TIRA KANDA YA KATI YAKAMATA BIMA FEKI KATIKA VYOMBO VYA MOTO DODOMA

Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Kati, Stella Rutaguza akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mjini Dodoma kuhuasiana na ukaguzi uliofanyuwa na mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na kufanikiwa kukamata magari 15, pikipiki na bajaji ambazo zilikuwa zinatumia Bima feki.(Picha na Mroki Mroki).
**************
 Na Anastazia Anyimike, Dodoma
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kanda ya Kati, imekamata magari 15 yakiwemo ya abiria kutokana na kukutwa na bima feki huku wananchi wakitakiwa kuhakiki bima hizo kabla ya kuondoka kwenye ofisi walizonunulia.

Akizungumza jana Meneja wa TIRA kanda ya Kati, Stella Rutaguza alisema katika operesheni iliyofanyika kwa siku tatu mkoani hapa kuanzia Febbruari 26 mwaka huu, imefanya kukamatwa kwa mahari 14 zikiwamo daladala na costa inayofanya asafari zake kati ya Dodoma na Morogoro na magari binafsi.

Alisema katika msako huo  ambao alisema ni endelevu ulihusisha ukaguzi wa magari 586, umewezesha kukamata bajaj tano na pikipiki mbili na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja ambaye amehusika kuuuza bima feki.

" Operesheni hii ni endelevu, tunataka kukomesha hali hii ambayo ni hatari kwa watumiaji wa vyombo vya moto na pia uhalifu ambao unalikoseshea taifa mapato," alisema.

Alisema katika operesheni hiyo wamebaini kuwa kuna wale ambao wananunua bima feki wakiwa wanajua ambao wamekuwa wakiuziwa kati ya Sh 5,000 hadi 10,000 kwa stika ya bima yenye thamani kuanzia laki tatu na kuendelea.

" Pia wapo ambao wanauziwa stika za bima feki wakiwa hawajui, na wanauziwa kwa thamani ya fedha ambazo serikali imeweka kulingana na aina ya bima na aina ya chombo cha usafiri," alisema.

Rutaguza amewataka wananchi kuhakikisha wanakagua na kuthibitisha kama bima waliyokata kuwa ni halali wakiwa kwenye ofisi walizokata na kuondokana na tabia ya kulipia bima ka wanaouza bima ambao wanazunguka nazo mtaani.

" Kuna watu wawili tuliwakamata wanasema hawajui waliowauzia bima walikutana na watu hao wakiwa gereji, watu hao bado tunawashikilia kwa sababu haiwezekani stika ya bima amya ni nyaraka muhimu ikauzwa mikononi na wewe ukanunua," alisema


Wednesday, 28 February 2018

TRENI YA ABIRIA DODOMA-KIGOMA KUPITIA TABORA YAPATA AJALI UVINZA

Treni ya abiria iliyokuwa safarini kutoka Dodoma kwenda Kigoma kupitia Tabora imepata ajali katika eneo la kijiji cha Mpeta, Wilayani Uvinza mkoani Kigoma hii leo baada ya kichwa kuacha njia na mabehewa mawili kuanguka.


JAPAN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 77.3 KUJENGA NEW BAGAMOYO ROAD DAR ES SALAAM

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (kulia), na Balozi wa Japan nchini,  Masaharu Yoshida, baada ya tukio la kusaini mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 77.3 zilizotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya Mradi wa upanuzi wa  Barabara ya njia ya nne ya New Bagamoyo Road kutoka Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,  Doto James, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa tukio la kusaini mkataba wa msaada wa Shilingi bilioni 77.3 zilizotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili yaMradi wa upanuzi wa Barabara ya njia nne ya New Bagamoyo Road kutoka Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam. Anayeangalia makaratasi nyuma ni Balozi wa Japan nchini,  Masaharu Yoshida.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).
***********************
Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), imeipatia Tanzania ruzuku ya Yen bilioni 3.78 sawa na Shilingi bilioni 77.3 kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya New Bagamoyo, kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.

Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini leo Februari 28, 2018, Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida na kushuhudiwa na Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Toshio Nagase na Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Barabara nchini-Tanroads, Mhandisi Patrick Mfugale.

Mradi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.3 utahusisha barabara yenye njia nne pamoja na kuanza kwa awamu ya nne ya ujenzi wa barabara itakayotumiwa na mabasi ya mwendo wa haraka (BRT phase IV).

Akizungumza baada ya kutiwa saini wa makubaliano hayo, Doto James amesema kuwa barabara hiyo ikikamilika itasaidia  kutatua changamoto ya msongamano wa magari yanayotoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

"Upanuzi wa Barabara ya New Bagamoyo si tu kwamba utaondoa msongamano wa magari, bali pia ni kiungo muhimu cha Bandari ya Bagamoyo ambayo itarahisisha usafirishaji wa abiria, mizigo na huduma kutoka Jiji la Dar es Salaam, mkoa wa Pwani na mikoa mingine nchini" Alisema  Doto James.

Ameishukuru Japan kwa msaada mwingine uliotolewa mwezi Septemba, 2017 wa kiasi cha fedha za Japan (Yen) milioni 69 sawa na shilingi bilioni 1.4 ambazo zimetumika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa barabara hiyo itakayoanza kujengwa

James ameeleza kuwa  awamu ya kwanza, Japan ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 99.5. kujenga barabara ya njia nne katika kipande cha kilometa 12.9 kutoka makutano ya barabara ya Tegeta na makutano ya barabara ya Mwenge pamoja na kukamilisha ujenzi wa madaraja ya Mlalakuwa, Lugalo na Tegeta.

“Si mara ya kwanza kwa Japan kuisaidia Tanzania, wanajenga barabara za juu katika makutano ya Tazara, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Dodoma hadi Babati mkoani Manyara (km 188.15), Tunduru-Mangaka – Mtambaswala (km 202) na barabara ya Iringa hadi Dodoma (259.9)” alisisitiza  Doto James.

Balozi wa Japan, Mhe. Masaharu Yoshida ameeleza kuwa kutolewa kwa msada huo ili kuwezesha awamu ya pili ya ujenzi wa barabara kuanza kutayafanya matokeo ya kujenga barabara hiyo kuanza kuonekana dhahiri ikiwemo kupunguza msongamano wa magari kwa kiasi kikubwa ili kuokoa fedha nyingi zinazotokana na changamoto za msongamano huo.

"Ili kukamilisha usanifu wa kina wa mradi huu, nilisaini mkataba wa usanifu wa kina wa mradi wa upanuzi wa barabara ya new Bagamoyo  (Awamu ya Pili) miezi mitano iliyopita, hatimaye sasa ninasaini mkataba wa sehemu kuu ambayo ni ujenzi wenyewe" Alisema Balozi Yoshida.

Balozi huyo wa Japan hapa nchini, amesema mradi huo utasaidia kuboresha ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini nchini na kwamba msaada huo ni mwendelezo wa kudumisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Japan na Tanzania.

Utafiti uliofanyika hivi karibuni unaonesha kuwa Barabara ya Bagamoyo ndiyo yenye msongamano mkubwa wa magari  yanayokadiriwa 52,000 yanayopita kila siku katika barabara hiyo.


LUNDENGA AJITOA KUANDAA MISS TANZANIA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Ageny, Hashim Lundenga akizungumza na waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo ambapo alitangaza rasmi kampuni hiyo kujitoa katika uandaaji wa shindano Miss Tanzania  tangu Februari 2018. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basila Mwanukuzi ambao ndio watakuwa waandaji wapya wa Miss Tanzania. Kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mwingereza.
Mashindano ya Miss Tanzania kuanzia sasa yatakuwa yakiandaliwa na Kampuni ya The Look Company Limited, inayoongozwa na Mwanadada Basila Mwanakuzi aliyepata kuwa Miss Tanzania 1998. 

 Kampuni ya Lino Intentional Agency Limited imekuwa waandaaji wa shindano la Miss Tanzania tangu mwaka 1994 na katika kipindi hicho inajivunia kutwaa taji la Miss World Africa 2005 kupitia Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari