Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday, 22 February 2018

RAIS WA FIFA AKIWA NCHINI TANZANIA LEO

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino (aliyevaa shuka la kimasai) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania Leodger Tenga mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) wakiwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) wakiangalia bidhaa mbalimbali za uchongaji na ushonaji toka kwa wajasiriamali wa Tanzania kabla ya kuanza kwa kikao cha shirikisho hilo mapema hii leo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino (katikati) akiwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika Ahmad Ahmad na kulia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania Wallace Karia.
Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino (aliyevaa shuka la kimasai) akivalishwa urembo wa mkononi wenye rangi za bendera ya Taifa mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano Mkuu toka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Tengeneza (kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino, zawadi mbalimbali toka bodi hiyo kabla ya kuanza kwa mkutano wa shirikisho hilo mapema hii leo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Picha na Idara ya Habari - MAELEZO


DK. KIGWANGALLA AAGIZA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI WAMIMBIKI IPANDISHWE HADHI KUWA PORI LA AKIBA



Na Hamza Temba - WMU-Bagamoyo, Pwani
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi kuanzisha mchakato wa kisheria wa kupandisha hadhi Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wamimbiki kuwa Pori la Akiba ili iweze kuhifadhiwa vizuri baada ya kushindwa kujiendesha.

Ametoa agizo hilo leo mkoani Pwani baada ya kutembelea eneo la Jumuiya hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi katika eneo hilo ambalo ndani yake pia kuna mapito ya wanyamapori.

Dk. Kigwangalla amechukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa jumuiya hiyo ikiwemo tuhuma walinzi wake kutoka katika vijiji vinavyounda jumuiya kujihusisha na vitendo vya ujangili. Hata hivyo alipokea ombi la Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Omari Tofiki ambaye aliiomba Serikali ichukue jukumu la kulinda hifadhi hiyo kwa asilimia 100. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


Tuesday, 20 February 2018

MAKAMU WA RAIS AZINDUA BARABARA YENYE JINA LAKE BARIADI


MGWIRA AFUNGUA MAFUNZO YA MADAKTARI YALIYOANDALIWA NA WCF

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira, akifungua mafunzo ya siku tano ya kufanya tathmini ya Mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini mjini Moshi Februari 19, 2018.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amewataka madaktari na watoa huduma za afya, wanaohuduria Mafunzo ya siku tano, (5), ya kufanya tathmini ya Mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi, kuzingatia miiko ya kazi zao wanapotekeleza jukumu hilo.
 
 Mkuu wa Mkoa aliyasema hayo Februari 19, 2018, wakati akifungua mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF) na kuwaleta pamoja madaktari zaidi ya 200 wa Kanda ya Kaskazini na kufanyika Mjini Moshi.

Alisema, lengo la Mafunzo hayo, ni kuwajengea uwezo Madaktari ili hatimaye watoe huduma kwa weledi na kwa urahisi kwa wafanyakazi wanaopatwa na madhara wawapo kazini katika maeneo mbalimbali nchini. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


DAWASA NA DAWASCO ZATAKIWA KUPELEKA HUDUMA ZA MAJI PEMBEZONI MWA JIJI LA DAR



Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso (wa pili toka kulia) akiwa na katibu tawala wa Wilaya ya Temeke, Edward Mpogolo wakati wakipatiwa maelezo machache juu ya uharibifu wa miundo mbinu ya maji inayofanywa na wananchi wasio waaminifu wakati wa ziara ya Naibu huyo aliyoifanya katika manispaa ya Temeke na Ilala ili kujionea miradi mbali mbali ya maji.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso akiangalia moja ya mradi wa maji.
 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso amezitaka mamlaka zinazohusika na usambazaji wa huduma ya maji safi na taka (DAWASA na DAWASCO) kuendelea kusambaza huduma pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.

Kauli hiyo ameitoa Februari 19, 2018 jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake aliyoifanya katika manispaa ya Temeke na Ilala ili kuweza kujionea miradi mbali mbali iliyoanzishwa ili kuweza kuwafikia huduma ya maji kwa urahisi.


Monday, 19 February 2018

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI JIMBO LA BUSEGA


Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Kiloleli ambao utafaidisha vijiji vitatu, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Busega Dkt. Raphael Chegeni.

Mbunge wa Jimbo la Busega Dkt. Raphaele Chegeni akimshukuru Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan baada ya kuweka jiwe la msingi kla mradi huo wa maji. katikati yao ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka.

Makamu wa Rais , Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Masanza Kona, Kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

Mbunge wa Jimbo la Busega Dkt. Raphaele Chegeni akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati wa kusalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi barabarani eneo la Nyashimo kumsalimia Makamu wa Rais ambaye ameanza ziara ya siku tano mkoani Simiyu.


Saturday, 10 February 2018

ORODHA YA MAJINA YA WATUMISHI WA UMMA WANAOSTAHILI KULIPWA MADAI YA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA HAYA HAPA

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango

ORODHA YA MAJINA YA WATUMISHI WA UMMA WANAOSTAHILI KULIPWA MADAI YA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA


RAIS DKT. MAGUFULI AWAANDALIA MABALOZI SHEREHE YA MWAKA MPYA MABALOZI WANAOWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI (DIPLOMATIC SHERRY PARTY) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kuwakaribisha Mabalozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam Ijumaa jioni Februari 9, 2018 kabla ya kuanza kwa hafla ya kukaribisha mwaka mpya kwa Mabalozi hao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kuwakaribisha Mabalozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam Ijumaa jioni Februari 9, 2018 kabla ya kuanza kwa hafla ya kukaribisha mwaka mpya kwa Mabalozi hao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kuwakaribisha Mabalozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam Ijumaa jioni Februari 9, 2018 kabla ya kuanza kwa hafla ya kukaribisha mwaka mpya kwa Mabalozi hao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kuwakaribisha Mabalozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam Ijumaa jioni Februari 9, 2018 kabla ya kuanza kwa hafla ya kukaribisha mwaka mpya kwa Mabalozi hao. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.


Thursday, 8 February 2018

WAZIRI MWIGULU AONGOZA OPARESHENI YA KUTEKEZA BANGI ARUSHA

Waziri wa mambo ya ndani nchini,Dk Mwigulu Nchemba ameongoza oparesheni ya kuteketeza jumla ya ekari  sita za bangi zilizokuwa zimelimwa katikati ya msitu ndani ya kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Mwigulu akishirikiana na Kamanda wa Polisi Arusha, Naibu Kamishna wa Polisi, Charles Mkumbo pamoja na askari polisi mkoani humo walilazimika kuacha magari yao njiani na kutembea umbali wa kilomita 5 milimani kufika katikati ya msitu huo ambapo wamiliki wa mashamba hayo walitokomea kusikojulikana.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mwigulu alisema kwamba serikali itaendelea na oparesheni pande zote za nchi na haitasita kuwakamata wahusika wote na kutaifisha magari yatakayotumika kusafirisha bangi.

Akizungumza na askari waliokuwa wakishiriki katika zoezi hilo Mwigulu mbali na kuwapongeza kwa kazi wanayofanya lakini aliwambia kwamba pamoja na kufanikiwa kuteketeza madawa ya kulevya yanayolimwa mashambani lakini waongeze juhudi pia katika kupambana na madawa ya kulevya yanayotengenezwa viwandani.

“Niwapongeze sana songeni mbele na kazi ya kukamata madawa yote ya kulevya mmefanya kazi kubwa sana ya kukabiliana na madawa ya kulevya yanayolimwa mashambani ongezeni bidii kukamata na yale yanayozalishwa viwandani”aliwaambia Mwigulu

Nae RPC Mkumbo alisema jumla ya ekari sita za mashamba ya bangi zimeteketezwa na kusisitiza kwamba oparesheni hiyo ni endelevu katika mkoa wa Arusha na wilaya zake.

Mkumbo,alifichua mbinu mpya wanayotumia wamiliki wa mashamba hayo kwamba kwa sasa wameamua kulima mashamba hayo katikati ya misitu kwa lengo la kujificha ili kukwepa mkono wa sheria.

“Walidhani kulima bangi katikati ya misitu hatutawakamat sisi tuna mbinu nyingi na hatutakubali kuona vijana wetu wanaharibikiwa kwasababu ya bangi”alisema Mkumbo.


JKCI YAWAPA SOMO WABUNGE KUHUSU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea mpango wa Serikali kupitia Hospitali za mikoa wa kusomesha madaktari bingwa wengi ili kuweza kukabiliana na uhaba wa wataalam hao wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba.
Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa akiwasisitiza wabunge wenzake umuhimu wa kupima afya zao hasa tezi dume kwa wanaume wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Mbunge wa Bunda mjini, Ester Bulaya akieleza jinsi anavyoridhishwa na huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na JKCI ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisalimiana na Daktari wa Bunge Jeminian Temba mara baada ya kumalizika kwa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Katikati ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Yona Gandye. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


Wednesday, 7 February 2018

PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100: UHAMIAJI

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dkt. Anna Makakala akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu. 
 IDARA ya uhamiaji nchini imewataka watanzania kupuuza habari zinazozagaa kuhusu uvumi wa pasipoti mpya kuwa zimechakachuliwa.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dkt. Anna Makakala amesema wananchi wanatakiwa kupata taarifa sahihi kila mara juu ya kila jambo linalohusu maendeleo yao na mambo yanayoletea ustawi wa Taifa letu,sisi ndio wenye taarifa sahihi zinazohusu Mchakato mzima wa Pasipoti Mpya za Kielektroniki

Hivi karibuni Rais Dkt. John Magufuli wakati akizindua hati mpya za kusafiria alisema kumekuwapo na wahujumu wa mchakato huo ambao hawakufanikiwa kuiba sh. bilioni 400.

Amesema kumekuwapo kwa watu waliozunguka kila kona na kutumia kila njama zote kupiga vita mchakato huo wakidhani watafanikiwa kuhujumu serikali.

Dkt. Anna Makakala amesema hatua hizo za kutoa na kueneza taarifa zisizo sahihi zinawaletea mkanganyiko wananchi na kudhoofisha mawazo na fikra chanya kwa Taifa lao

Amesema ni vyema jamii kutambua kuwa mchakato wa Pasipoti mpya ya kidigitali ni hatua kubwa kwa Taifa hili na si vyema kuutolea Taarifa zisizo sahihi, amewasihi wanahabari kupata taarifa kutoka katika vyanzo sahihi na kuzifikisha kwa walaji ambao ni Wananchi," 

Amesisitiza hatua ya mafanikio ya matumizi ya hati hizo hazitarudi nyuma kwa sababu ya kuwapo na taarifa zisizo sahihi zenye lengo la kupotosha ukweli wa mchakato huo.

“Ni vyema jamii kuelewa kazi ya hati hizo ni kulinda usalama wa nchi yetu hivyo Uhamiaji tutaendelea kudhibiti mipaka ya Tanzania na kulinda usalama wa nchi kwa kuwezesha jamii na raia wa kigeni kufuata taratibu katika utokaji,ukaaji na uingiaji wa kila mmoja,” amesema Dkt. Makakala.
Amesema kila nchi yenye kuhitaji maendeleo ni muhimu kutumia hati ya kusafiria ya kielektroniki ili kufikia mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

“Mabadiliko ya kidunia katika maendeleo yanatuonyesha wazi kuwa Taifa hili limefikia kuwa na hati za kisayansi na kiteknolojia hivyo katika hati mpya,mtu yeyote hataweza kutumia ujanja au kughushi na kutumika kwa matumizi yasiyo sahihi,” amesema Dkt. Makakala.

Amesema anaamini idara hiyo haitashindwa na wachache wanaokubali kutumika kuhujumu mchakato huo kwa maslahi binafsi kwakuwa kushindwa kwa mchakato huo ni kupunguza hadhi ya usalama wa nchi.

“Pasipoti ndio kitu kinachotuwezesha kudhibiti wanaoingia nchini na kutoka hiki ni kitambulisho cha raia sehemu yoyote duniani wenye Pasipoti za Tanzania ni mabalozi wa Tanzania mfumo huu utawezesha kudhibiti ujanja wote unaotumika kutakuwa na cheap na security features nyingi sifa ya Taifa letu dunia imeharibika lazima kufanya maamuzi kwa maslahi ya Taifa letu,” amesema.

Dk. Anna alisema kufanikiwa kwa mradi huo wa e-Immigration kwa gharama ya dola za Marekani milioni 57 imekuwa mwiba kwa vigogo walioondolewa Uhamiaji na sasa wanahaha kwa aibu wakidai kwamba gharama iliyotajwa ni kwa ajili ya mradi mradi mmoja tu wa e-Pasipoti.

“Ni wajibu wa kila mtanzania kuwa macho na wale wote wanaotumiwa na mafisadi kwa ajili ya kuichafua serikali kwakuwa imezuia na kupambana na uhujumu uliotaka kujitokeza,” amesema.

Amesema hati hizo zitawezesha waliopotelewa na hati zao kutumia mfumo wa kiteknolojia na kupakua app yake hata katika simu ya mkononi, hivyo kutambulika na kupewa msaada haraka kokote duniani.

Amesema hati hiyo inaviwango vyote vya ubora wa kimataifa pia itatumika kama kitambulisho kwa nchi za Afrika Mashariki.


Monday, 5 February 2018

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WIZARA YA NISHATI Mh.SUBIRA MGALU MKOANI KILIMANJARO

Tarehe 24 - 26/01/2018 Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametembelea na kukagua utekelezaji wa Miradi ya umeme vijijini (REA II & REA III) kwenye jumla ya vijiji 18 katika wilaya za ROMBO, MWANGA NA SAME Mkoani Kilimanjaro.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliongea na wananchi, pia kutambulisha wakandarasi wa miradi ambapo aliwaagiza wakandarasi waepuke kurudia makosa yaliyojitokeza awali na kuhakikisha wanakamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa.

Pia Katika ziara hiyo Mh. Naibu waziri alitembelea bwawa la kuzalisha umeme la NYUMBA YA MUNGU kujionea shughuli za uzalishaji.

Mh Naibu waziri amemaliza ziara yake 26/01/2018 saa 12:00 jioni na kuelekea mkoani TANGA.

RCRO KILIMANJARO.

Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwaeleza wananchi wa kijiji cha Mkisha kuhusu kifaa kijulikanacho kama UMETA (REDY BODY) kifaa hicho hutumika kama mbadala wa kusuka mifumo ya waya (wiring) ndani ya nyumba. Aliyeshika kifaa hicho ni Afisa uhusiano TANESCO KILIMANJARO Bw. Samuel Mandari.

 Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasikiliza wanakijiji na kueleza uhitaji wa huduma ya umeme.

Wanakijiji wakimsikiliza Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) akieleza uhitaji wa huduma ya umeme.


Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Mkuu wa wilaya ya Same Mh. Rosemary Senyamule, Kamati ya Ulinzi na usalama wilaya, wakiwa na viongozi wa TANESCO MKOA wa Kilimanjaro walipo tembelea Kijiji cha Vunta wilayani Same.


Saturday, 3 February 2018

COASTAL UNION YAPOKELEWA KISHUJAA,WAZIRI UMMY,RC SHIGELLA WAONGOZA MAPOKEZI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwasalimia wakazi wa Mji wa Pongwe mara baada ya kuwasilia na timu ya Coastal Union ikitokea mkoani Morogoro ambapo iliweza kupanda daraja baada ya kuifunga Mawenzi ya Morogoro mabao 2-0 kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kulia akizungumza wakati alipoipokea timu ya Coastal Union mara baada ya kupanda daraja kucheza Ligi kuu msimu ujao mapokezi hayo yalifanyika kwenye eneo la Pongwe Jijini Tanga kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akizungumza katika mapokezi hayo 


Wapenzi wa soka mkoani Tanga pamoja na wananchi wakiwa wamezingira barabara ya Tanga kwenye mikoani eneo la Pongwe wakiilaki timu ya Coastal Union leo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akizungumza katika mapokezi hayo akizungumza katikani ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella 
Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union,Steven Mguto katikati akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa kamati ya usaji wa klabu hiyo Ahmed Aurora kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Tanga(TRFA) Saidi Soud.
Mfungaji wa moja ya mabao yaliyoipandisha timu ya Coastal Union Athumani Iddi Chuji akizungumza kwenye mapokezi hayo leo (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)


Friday, 2 February 2018

TRA yafunga hoteli, kituo cha mafuta kwa deni la Sh1bn

Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoani Mtwara  imezifungia hoteil tatu pamoja na kituo cha kuuza mafuta kwa kushindwa kulipa malimbikizo ya kodi zaidi ya Sh bilioni 1.

Hotel zilizofungiwa ni Naff Beach, Naf blue na BNN wakati kituo cha mafuta  kilichofungiwa  pamoja na kituo cha mafuta kijulikanacho kwa jina la  Mnarani Petrol Station.

Afisa mwandamizi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi mkoa wa Mtwara, Flavian Byabato amesema zoezi hilo ni endelevu kwa mkoa mzima.

“Ni madeni ambayo yametokana na ukaguzi kwa kipindi cha miaka mitatu nyuma, kikubwa walipe kodi..tunafungia kwa mambo mbalimbali kama malimbukizo ya madeni ya muda mrefu, matumizi sahihi ya mashine za EFD katika kutoa na kudai risiti sahihi inayoakisi gharama halisi ya malipo na kutii sharia za kodi kama kutunza kumbukumbu,” amesema Byabato

Byabato ameongeza kuwa endapo wadaiwa watashindwa kulipa madeni yao, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.


YALIYOJIRI BUNGENI LEO FEBRUARI 02, 2018

Wabunge Ruth Mollel, Mary Nagu na Angellina Malembeka wakiwasili bungeni kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Bunge, mjini Dodoma.
/Picha: Katuma Masamba-Daily News Digital

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakiwasili bungeni kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha nne cha mkutano wa 10 wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.

Wabunge wakiwasili bungeni kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Bunge, mjini Dodoma.

Wabunge wakijadiliana wakati wa kikao cha Bunge mjini Dodoma

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akijibu swali bungeni, mjini Dodoma.


JPM aguswa na kifo cha mwanasiasa Kingunge

Na Mwandishi Wetu
RAIS Dkt. John Magufuli amepokea kwa huzuni na masikitiko taarifa za kifo cha mmoja wa waasisi wa Taifa na mwanasiasa mkongwe nchini Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kilichotokea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam mapema leo Ijumaa, taarifa ya Ikulu yaeleza.

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na mbwa wake nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam Desemba 22, 2017.

Taarifa iliyosambazwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais imemnukuu Dkt. Magufuli akisema staifa limempoteza mtu muhimu ambaye alitoa mchango mkubwa katika juhudi za kupigania uhuru na baada ya kupata uhuru akiwa mtumishi mtiifu wa Chama cha TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM), na katika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya Serikali.

“Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ametoa mchango mkubwa sana, sisi kama Taifa hatuwezi kusahau na tutayaenzi mema yote aliyoyafanya wakati wa utumishi wake uliotukuka, ametuachia somo la kupigania maslahi ya nchi wakati wote, kuwa wazalendo wa kweli, kudumisha amani na mshikamano, kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kuwa na nidhamu” amesema Mhe. Magufuli.

Hata hivyo, Rais Magufuli amewapa pole wanafamilia wote, wanachama wa CCM, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu, na amewaombea kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi.