Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 8 February 2018

JKCI YAWAPA SOMO WABUNGE KUHUSU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea mpango wa Serikali kupitia Hospitali za mikoa wa kusomesha madaktari bingwa wengi ili kuweza kukabiliana na uhaba wa wataalam hao wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba.
Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa akiwasisitiza wabunge wenzake umuhimu wa kupima afya zao hasa tezi dume kwa wanaume wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Mbunge wa Bunda mjini, Ester Bulaya akieleza jinsi anavyoridhishwa na huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na JKCI ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisalimiana na Daktari wa Bunge Jeminian Temba mara baada ya kumalizika kwa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Katikati ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Yona Gandye. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Wabunge wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) akielezea kuhusu dalili za shinikizo la damu na tiba yake wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. 
***************
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Wazazi wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo zote zinazotakiwa ili waweze kuepukana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo.

Rai hiyo imetolewa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akiongea na wabunge waliohudhuria semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.


Waziri Ummy aliwaomba wabunge hao kila wanapokutana na wananchi kupitia mikutano ya hadhara wawasisitize umuhimu wa kuwapeleka watoto wao katika vituo cha afya ili wakapate chanjo zinazohitajika kwa wakati.

Aidha Waziri huyo alisema kuwa matibabu ya moyo pamoja na magonjwa mengine yasiyoambukiza ni ya gharama kubwa na kuwaomba wabunge hao kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao utawasaidia kupata matibabu katika Hospitali zote nchini ikiwemo JKCI na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Katika hatua nyingine Mhe. Ummy aliwataka wakurugenzi wa Taasisi zingine kuiga mfano wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed ambaye kupitia uongozi wake na jitihada zake binafsi Taasisi hiyo imeweza kutoa huduma bora na kuwahudumia wananchi
vizuri katika matibabu ya moyo na hivyo kuokoa maisha ya watanzania wengi.

“Katika utendaji kazi wa Taasisi hii tunaona juhudi binafsi za kiongozi ambaye kwa jitihada zake amewatumia marafiki aliosoma nao na kufanya nao kazi katika nchi mbalimbali kuja nchini kutoa mafunzo kwa wataalam wetu na huduma za matibabu magumu ya moyo ambayo sisi
peke yetu tusingeweza kuyafanya kutokana na uchanga tulionao”, alisema Waziri Ummy .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Maendeleo ya Jamii  Peter Serukamba aliomba katika kikao cha Bunge la Bajeti wabunge wapewe semina kama hiyo ambayo itaenda sambamba na upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo moyo, saratani za matiti na shingo ya
kizazi, tezi dume na kisukari.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi aliwasisitiza wabunge kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kama watakutwa na matatizo waweze kupata matibabu kwa wakati, kufanya mazoezi na kuepuka kula vyakula ambavyo vitawaepusha kupata
magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

Katika semina hiyo ya siku moja mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwa ni pamoja na Shinikizo la damu na dalili zake na tiba , kiharusi, tezi dume na wanawake kukoma kwa hedhi kwa wanawake.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment