Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday 19 August 2017

MAKONDA APIGA MARUFUKU WATENDAJI WA MKOA KUSAFIRI NJE YA MKOA WA DAR BILA RUHUSA YAKE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepiga marufuku watendaji wa Mkoa huo kutoka nje ya mkoa bila kutoa taarifa kwa mkuu wa Mkoa

Makonda amepiga marufuku hiyo leo wakati wa kongamano la tathimini ya hali ya miundombinu ya barabara za mkoa huo unaoendelea katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.

Kauli hiyo ya Makonda imekuja baada kukosekana kwa watendaji ambao walitakiwa kuhudhuria kongamano hilo kwa madai kuwa wako nje ya mkoa kikazi huku waliobakia wakishindwa kueleza kuwa wapo kwaajili ya kazi gani.

" Kuanzia sasa hakuna mtumishi wa Mkoa huh kutoka nje bila kutoa taarifa hata kama ni kazi ya Wizara gani lazima mtoe taarifa, kumekuwa na tabia ya watu kujitengenezea tu safari ambazo hazijulikani wakati hata rais wetu alishazikataza," alisema Makonda.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment