Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Sunday 20 August 2017

MAKONDA AWAONGEZEA NGUVU TBC

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo ametoa msaada wa Gari aina ya Noah,Pikipiki Tatu, Komputer Tano na Camera Mbili za kisasa kwa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC ili kuongeza nguvu katika kuwafikia Wananchi.

Mbali na Vifaa hivyo vya kisasa pia Makonda amefanikiwa kumpata mfadhili atakaepaka Rangi Jengo lote la TBC kuanzia siku ya kesho ili liwe na mwonekano wa kisasa.u

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo Makonda amesema lengo ni kuwawezesha Wananchi ambao hawana uwezo wa kuita vyombo vya habari na kueleza matatizo yao waweze kufikiwa.

Makonda ametoa msaada huo baada ya kufika Ofisi za TBC na kubaini uwepo wa changamoto za vifaa ikiwemo Usafiri, Camera na Computer ambapo kwa sasa Gari na Pikipiki hizo zitawawezesha Waandishi kufika kwenye matukio kwa uharaka huku Compute zikimuwezesha  M
Wahariri kutekeleza majukumu yao.

Vifaa hivyo vitatumika kuongeza nguvu kwenye kipindi cha Hadubini ambacho kimekuwa kikisaidia Wananchi wanyonge kupaza sauti zao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TBC Martha Swai amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwapatia msaada huo kuku Zaitun Mkwama ambae ni mtayarishaji wa kipindi cha Hadubini akieleza kuwa vifaa hivyo vitawaongezea ufanisi katika kazi yao.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment