Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday 8 May 2017

MIILI YA WANAFUNZI 32, WALIMU 2 NA DEREVA WA SHULE YA LUCKY VICENT WALIOKUFA AJALINI YAAGWA

 HAKIKA ilikuwa siku ya majonzi makubwa kwa maelfu ya wakazi wa Arusha na viunga vyake pamoja na wale kutoka mikoa mbalimbali ya jirani na nje ya Tanzania wakati wa utoaji heshima kwa miili ya wanafunzi 32, walimu wa wili na dereva wa basi walilokuwa wakisafiria wanafunzi hao kutoka Kwa Mromboo Arusha kuelekea Karatu kupata ajali Mei 6,2017.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, ndiye aliyoongoza utoaji huo wa heshima za mwisho ulifanyika kitaifa katika Uwanja wa Mpira wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo.

Makamu wa Rais amewataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani na waache kutumia pombe na dawa za kulevya ili kuepukana na ajali ambazo zinagharimu maisha ya wananchi.

Makamu wa Rais pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta na Wakenya kwa ujumla kwa kuungana na Wananchi wa Tanzania katika msiba uliotokea.Katika kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dereva katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha, Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta amewakilishwa na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo Fred Matiang'i.

Ibada na Dua ya kuaga miili hiyo, imehudhuriwa na Mawaziri mbalimbali ikiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohammed Aboud,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene, Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Viongozi wa vyama vya siasa na Viongozi wa Dini.
 Maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakishusha miili ya marehemu tayari kwa kutolewa heshima za mwisho.
  Maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakishusha miili ya marehemu tayari kwa kutolewa heshima za mwisho.
 Ilikuwa ni majonzi makubwa si tu kwa wafiwa bali hata kwa wananchi wengine nao waliangua vilio na kuonesha ni jinsi gani wameguswa na msiba huo mzito kwa wana Arusha na Taifa kwa ujumla.
 Wanafunzi wa St Lucky Vicent ya Jiji Arusha wakiwa wenye huzuni kwa kuondokewa na wapendwa wao.
 Wazazi walilia sana na wengine kuanguka na kupoteza fahamu. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.

Majonzi na uchungu wa kuwapoteza wapendwa wao uliwafanya watu wengi kuzimia na watu wa huduma ya kwanza kuwasaidia kwa haraka.
 Viongozi mbalimbali walio hudhuria.
 Mwenyekiti wa Chadema na Mbumnge wa Hai, Freeman Mbowe akitoa salamu za Chama.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa salamu za rambirambi.
 Waziri Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza.
 Viongozi wa Upinzani wakitoa  heshima za mwisho.
 Mrembo Joketi Mwegelo nae alikuwepo kutoa heshima za mwisho.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt Ave Maria Semakafu akiweka shada.
 Mbunge Lazoro Nyalandu akipita na mkewe Faraja Kota kutoa heshima za mwisho.
 Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel nae akitoa heshima za mwisho.
Wananchi mbalimbali wakipita kutoa heshima za mwisho.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment