Nyaborogo Patrick Marwa, Mhasibu wa Afya Halmashauri ya
Wilaya ya Chamwino akichangia wakati wa mafunzo
ya mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha
kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting
and Reporting System – FFARS.
Mkuu wa kitengo cha Mifumo ya Fedha wa Mradi wa PS3, Dkt.
Gemini Mtei, akielezea lengo la
mafunzo ya mfumo mpya wa uhasibu na
utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial
Accounting and Reporting System – FFARS.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mfumo mpya wa uhasibu
na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility
Financial Accounting and Reporting System – FFARS wakifanya mafunzo kwa vitendo
baada ya maelekezo kutoka kwa wakufunzi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Mwezeshaji wa mafunzo ya mfumo mpya wa uhasibu na utoaji
taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial
Accounting and Reporting System – FFARS, Abdul Kitula, Mshauri wa Udhibiti wa
Fedha za Umma wa mradi wa PS3 akifundisha washiriki namna ya kutumia mfumo huo
***************
SERIKALI sasa itaanza kupeleka
rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo vya afya kwa ngazi za halmashauri ikiwa
ni moja ya jitihada za kuboresha huduma za afya kwa wananchi. Anaandika Mroki Mroki wa Daily News-Habarileo Blog.
Upelekaji wa Rasilimali Fedha
moja kwa moja kwa vituo vya kutolea huduma itahakikisha kuwa Fedha zinazotolewa
na Serikali zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Mkakati huu mpya wa kuboresha
sekta ya afya unatekelezwa kwa njia ya msaada kutoka Shirika la Maendeleo ya
Kimataifa la Marekani (USAID), kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta
za Umma (PS3).
Vituo vya kutolea huduma
ambavyo vitapokea fedha hizo vinajumuisha Zahanati, Vituo vya Afya, na
Hospitali za Wilaya. Zoezi hili ni
sambamba na inavyotekelezwa kwenye sekta ya elimu, Serikali za Vijiji na Ofisi
za Kata.
Mfumo huu mpya wa kupatiwa rasilimali
fedha utatoa motisha kwa vituo vya kutolea huduma za afya na kuongeza kipaumbele
cha utoaji huduma bora kwa wananchi wa Tanzania na kuongeza usawa na uwazi.
Aidha kupitia mfumo huo mpya wa
uhasibu na utoaji taarifa unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial
Accounting and Reporting System (FFARS) unasaidia utekelezaji wa utoaji wa
rasilimali fedha moja kwa moja kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma kwa
kuimarisha uhitaji wa kuwepo kwa usimamizi wa fedha katika ngazi ya vituo vya
kutolea huduma.
FFARS itawapatia watoa huduma
mfumo sanifu uliorahisishwa ambao utawawezesha kutunza taarifa za fedha zinazotolewa
na zilizopo katika vituo vyao.
FFARS itaweza kufuatilia matumizi
ya fedha hizo katika kufikia malengo ya utohaji huduma na kuhakikisha
yanaendana na sheria za manunuzi na utoaji taarifa. Taarifa hizi zitasaidia Serikali kuimarisha Mfumo
wa Usimamizi wa Fedha za Umma na kuongeza uwazi, na hivyo watoa huduma wa afya
kuwa na wajibu kwa jamii wanayoihudumia.
Sambamba na uzinduzi wa FFARS,
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la
Marekani (USAID), wameandaa mafunzo ya kina yatakayoanza mwezi huu kwa
wakufunzi 490 katika ngazi ya taifa na halmashauri, yatakayofanyika katika
mikoa minne nchini.
Mikoa ambayo itahusika katika
mpango huu ni Dodoma, Mbeya, Mtwara, na
Shinyanga, ambao utawawezesha watumishi katika vituo vya Afya na Elimu kupata ujuzi
wa namna ya kutumia mfumo mpya wa FFARS.
Wakufunzi wataweza kutoa elimu
ya utumiaji wa mfumo huo kwa watumiaji wa mwisho wa mfumo wa FFARS kwa zaidi ya
Vituo vya Afya 550, Zahanati 6800, Hospitali za Wilaya 135, na takribani Shule
za Msingi na Sekondari 20,000 katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, vikiwemo
vituo vya kutolea huduma kutoka Mikoa 13 na Halmashauri 93 zinazotekeleza Mradi
wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).
Mafunzo haya yatahakikisha
kuwa watoa huduma katika vituo wana ujuzi unaohitajika katika usimamizi wa
fedha na kutoa huduma bora kwa wananchi
wote Tanzania na kwa jamii zenye uhitaji.
Mwongozo huu wa FFARS upo
katika aina mbili: mfumo wa kielektroniki, na mfumo wa zamani ulioboreshwa wa kujaza
katika vitabu kulingana na miundombinu iliyopo katika vituo vya kutolea huduma Tanzania
nzima.
Ufahamu uliopo katika kutumia
mfumo wa zamani utasaidia uelewa wa haraka katika kutumia mfumo wa
kielektroniki, na baada ya uboreshwaji wa miundombinu tunatarajia vituo vyote
vitahamia katika mfumo wa kielekroniki.
Mfumo huu wa FFARS
unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI); Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi; na Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na USAID.
Mfumo utatumika katika vituo
vyote vya kutolea huduma ya afya na shule, na uhuishaji huu wa mfumo
utarahisishia na kuongeza ufanisi katika mifumo ya Serikali ya Tanzania na
kuboresha usimamizi na matumizi ya rasilimali za umma.
Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo
ya Sekta za Umma (PS3), ni wa miaka mitano na unatekelezwa katika mikoa 13 ya
Tanzania bara. PS3 inafanya kazi katika
sekta mbalimbali ili kuimarisha mifumo ya mawasiliano, utawala bora, fedha na
rasilimali watu, hususani kwa jamii zenye uhitaji.
Mfumo huu ni mzuri sana kwani utarahisha watumishi wanaosimamia raslimamli fedha katika vituo vya kutolea huduma kutoa taarifa kwa wakati na zilizo hahihi.
ReplyDeleteushauri hadi sasa bado watumiaji wa mfumo huu hawajawa na uwezo wa kuutumia kwa usahihi hii ni kutokana na wengi kutopata mafunzo ya kutosha namna ya kuutumia, baada ya mfumo huu kuboreshwa na kuwepo na chngamoto ya bakaa kuhama kutoka kwenye mifuko iliyobajetiwa na mfumo ulikubali na kuruhusu malipo kufanyika hata kama fedha hakuna. kwa sasa mfumo umetengemaa lakini wengi anashindwa kulipa kwa kuonekana hakuna fedha. Hivyo utatuzi umepatikana lakini wengi wanahoitaji mafunzo zaidi.
Nawapongeza wote waliotengeneza Mwongozo wa kufundisha FFARS kwa kutumia video nzuri kwa kweli nimejifunza na imenisaidia sana
ReplyDelete