Baadhi ya kazi ya sanaa za wanafunzi wa shule ya sekondari Mtoni
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mary Tesha akipanda mti katika madhimisho ya miaka 10 ya shule ya sekondari Mtoni
**************
Na
Alexander Sanga,Mwanza
Mkuu
wa wilaya ya Nyamagana Mary Tesha amewaomba wananchi na wadau mbali mbali
wajitokeze kwa wingi katika kuhakikisha wanachangia katika ujenzi wa maabara na
jengo la utawala katika shule ya sekondari ya Mtoni.
Akizungumza
katika madhimisho ya miaka kumi,tokea kuanzishwa kwa shule,Tesha amewaomba
wananchi wa kata ya Mabatini wahakikishe wanachangia kwa wingi ili kuhakikisha
ujenzi wa maabara na jengo la utawala linaanza mapema.
Tesha
alimuagiza diwani wa kata ya Mabatini Deus Lucas ahakikisha anawahamasisha
wakazi wa Mabatini wachangia katika ujenzi huo.Tesha alichangia shilingi
milioni 1.
Mwalimu
mkuu wa shule ya sekondari Mtoni Denis Mwakisimba alisema wanafunzi wa shuleni
wanapata changamoto kubwa katika kujisomea kutokana na ukosefu wa maktaba.
Mwakisimba
ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuleta vitabu 1200 vya masomo ya
sayansi.Mwakisimba alilamikia kuwepo kwa soko katika eneo la shule jambo
linalopelekea kuleta usumbufu wakati wanafunzi wakiwa masomoni.
Kwa
mujibu wa Mwakisimba alisema mpaka kukamilika kwa ujenzi wa maktaba na madarasa
jumla itagharimu shilingi milioni 250 Katika Harambe iliyofanyika shuleni hapo
wakazi wa Mabatini walichangia milioni 1.8.
Wadau
mbalimbali waliahidi mifuko ya Saruji 115,tofali 700 na tripu 5 ya mchanga.
Diwani
wa kata ya Mabatini,Deus Lucas alisistiza wakazi wa kata ya mabatini wajitoa
sana katika kuhakikisha wanajitoa kwa wingi ili kuleta maendeleo katika kata
yao.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment