Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sing'isi Bi.Faith Mushiro akionyesha
sehemu ambayo husababisha maji kujaa ndani ya madarasa pindi mvua
inaponyesha, wakatikati ni Mkurugenzi wa Benki ya biashara ya
Africa(CBA)Gifti Shoko pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo
sehemu inayovuja katika darasa
Mkurugenzi wa Benki ya biashara ya Africa(CBA)Gifti Shoko pamoja na timu yake wakikagua madarasa yanayojaa maji kipindi cha mvua
Na Pamela Mollel,Arusha
Shule ya msingi Sing’isi iliyopo katika wilaya ya Arumeru
Mkoani Arusha iliyokuwa ikikabiliwa na
changamoto ya madarasa kujaa maji imepatiwa msaada wa kiasi cha shilingi
Milioni nne na benki ya biashara ya Africa (CBA) kwaajili ya ukarabati wa
baadhi ya madarasa
Akikabidhi hundi katika shule hiyo juzi Mkurugenzi wa CBA
Gifti Shoko alisema kuwa lengo la msaadahuo ni kusaidia wanafunzi kuondokana na
changamoto ya kutoa maji katika madara pindi mvua zinaponyesha hali
inayosababisha kukosa vipindi viwili hadi vitatu kwa siku
Alisema kuwa msaada huo utumike kama ulivyo kusudiwa
kuboresha madarasa hayo kwani ubora wa elimu unaletwa na mazingira mazuri ya watoto kusomea
‘’Hapa nawaona Marais,
mawaziri wa kesho pamoja na wafanyakazi
wazuri wa bank yetu hivyo hatuna budi kutuoa msaada huu ikiwa kama mchango wetu
wa kuboresha sekta ya elimu na tunawahidi hatutaishia hapa tutaendelea
kuwasaidia kadri ya uwezo wetu ‘’
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Faith Mushiro akitoa neon la
shukrani alisema kuwa wanafunzi wa darasa la tano na la sita ndiyo hasa
walikuwa wakipata hadha hiyo ya kuondoa maji madarasani pindi mvua zinapoanza
kunyesha
Aidha alisema kuwa zaidi ya vipindi viwili hadi vitatu vya
asubuhi hushindwa kuhudhulia kutokana na changamoto hiyo hivyo kupitia msaada
huo wanafunzi watasoma katika vyumba vya
madarasa vizuri tofauti na kipindi cha nyuma
Awali akisoma Risala mwalimu wa shule hiyo Bw.Simon Mbawala kwa niaba ya shule hiyo alisema kuwa pamoja na
msaada waliopatiwa bado shule inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa makataba
ya kuhifadhi vitabu ,kuharibika kwa sakafu za madarasa pamoja na kupasuka kwa
vioo vya madirisha
Hata hivyo tunatoa shukrani zetu za dhati kwa mssada huu wa
ujenzi wa vyumba vinne ambayo vilikuwa na tatizo la kuvuja kwa maji kutokana na
bati zake kuwa chakavu hali iliyokuwa ikiwathiri sana wanafunzi na walimu hasa
ikifika wakati wa kufundisha
Mkurugenzi
wa Benki ya biashara ya Africa (CBA) Gifti Shoko akikabidhi hundi
ya kiasi cha shilingi Milioni nne kwa Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Sing’isi
iliyopo katika wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha juzi Bi.Faith Mushiro kwaajili
ya kukarabati madarasa manne ambayo hujaa maji kipindi cha mvua hali
ambayoilikuwa ikiwasababishia wanafunzi kukosa vipindi viwili hadi vitatu kwa
siku
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Sing'isi Bi.Faith Mushiro akitoa neno
la shukrani kwa uongozi wa benki ya CBA mara baada ya kupata msaada wa
shilingi Millioni nne kwaajili ya ukarabati wa madarasa
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment