Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 04
Aprili, 2017 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya Makatibu Wakuu.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais
Magufuli amemteua Prof. Kitila Alexander Mkumbo (pichani juu) kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maji na Umwagiliaji.
Prof.
Kitila Alexander Mkumbo anachukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba ambaye
amestaafu.
Kabla
ya Uteuzi huu Prof. Kitila Alexander Mkumbo alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM).
Mhe.
Rais Magufuli amemteua Dkt. Leonard Akwilapo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Kabla
ya Uteuzi huo Dkt. Leonard Akwilapo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Kufuatia
uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bi.
Maimuna Tarishi amehamishwa na kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge).
Bi.
Maimuna Tarishi anachukua nafasi iliyoachwa na Mussa Uledi ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.
Mhe.
Rais Magufuli amemteua Dkt. Ave Maria Semakafu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambako anajaza nafasi iliyoachwa na Dkt.
Leonard Akwilapo ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Kabla
ya Uteuzi huo Dkt. Ave Maria Semakafu alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya
na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Wateule
hao wataapishwa kesho tarehe 05 Aprili, 2017 saa 3:00 Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment