Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wafanyakazi katika kilele
cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa
Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe Mosi Mei, 2017 amesema
Serikali ya Awamu ya tano imepanga kufanya
nyongeza ya kawaida ya kila mwaka katika
mishahara yaani Annual increment,
ambayo ilikuwa imesimama kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na promosheni.
Rais Magufuli ametoa
ahadi hiyo katika Sherehe za siku ya Wafanyakazi duniani zilizofanyika katika
Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Amesema uamuzi wa
Serikali wa kuanza kutoa promosheni unatokana na kukamilika kwa zoezi la
uhakiki wa Wafanyakazi hewa zaidi ya
wafanyakzi kumi 19,000 walibainika kuwa wafanyakazi hewa.
''Yale mambo yote
yaliyokuwa pending ikiwa ni pamoja na promosheni kwa sababu tulishindwa, unaweza kupromoti mfanyakazi hewa hayupo,kwa
sababu tungetoa promosheni wakati kuna wafanyakazi 19,000 hewa,maanake
tungepromoti na 19,000 na siajabu na watu waliowaandika mule ndio wangeletwa
katika mapendkezo ya promosheni'' amesema Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli
amewaonya watumishi ambao wamekuwa wakidanganya umri wa kustaafu ili waendelee
kufanya kazi kwa muda mrefu na kuwa siku zao sasa zimekwisha.
Katika hatua nyingine
Rais Magufuli amepiga marufuku uhamisho wa Wafanyakazi bila kuwalipa stahili
zao kutokana na kuwepo na tabia ya kuwahamisha wafanyakazi bila kuzingatia
taratibu hasa za malipo ya uhamisho.
''Sasa niwaombe
wafanyakazi yeyote akihamishwa hakuna kuhama mpaka umelipwa pesa ya
uhamisho,kuanzia juu mpaka chini,yeyote atakaye kuhamisha mwambie nipe hela
yangu ya uhamisho ninapoenda akishindwa usihame kaa hapohapo ufanye kazi'' Amesema
Rais Magufuli.
Amesema viongozi
wengine wamekuwa wakiwahamisha wafanyakazi
kwa maslahi binafsi au visasi kutokana na maendeleo wanayowapata
wafanyakzi
Rais Mgufuli
amewahakikishia wafanyakazi kuwa Serikali ya awamu ya Tano itaendelea kuwajali
na kuwa karibu nao katika kutimiza dhana
ya utatu ya ushirikiano kati ya Serikali, Wafanyakazi na Waajiri kwa lengo la
kuleta maendeleo.
Aidha, Rais Magufuli amewaeleza
wafanyakazi mipango mbalimbali anayofanywa na Serikali katika kuwaletea
maendeleo ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege mpya ,ujenzi wa Reli ya kisasa,
utoaji elimu bila malipo na uboreshaji wa miundombinu katika kuwaletea
maendeleo wananchi.
Sherehe za Mei Mosi
zilizofanyika katika mkoa wa Kilimanjaro pia zimehudhuriwa na Makamu wa Rais
Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe.
Job Ndugai, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Wabunge na viongozi mbalimbali wa Chama
na Serikali ambapo kauli mbiu inasema,''
Uchumi wa Viwanda uzingatie kulinda Haki, Maslahi na Heshima ya Mfanyakazi''.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment