Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Monday, 19 June 2017

RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA YA SIKU TATU MKOANI PWANIRAIS Dkt. John Pombe Magufuli kesho Juni 20, mwaka huu anataraji kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoa wa Pwani.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jijini Dar es Salaam leo inaarifu kuwa katika ziara hiyo Rais Magufuli atazindua viwanda vikubwa vitano vilivyopo mkoani humo.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wake, Gerson Msigwa  imevitaja viwanda hivyo kuwa ni kiwanda cha vifungashio (Global Packaging Co. Ltd), kiwanda cha matrekta (Ursus-TAMCO Co. Ltd), kiwanda cha chuma (Kiluwa Steel Group), kiwanda cha kukausha matunda (Elven Agric Company) na atafungua kiwanda cha vinywaji baridi (Sayona Fruits).

Aidha Rais Magufuli atazindua mradi wa maji wa Ruvu na barabara ya Bagamoyo – Msata.

Rais Magufuli pia atapata fursa ya kukutana na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara iliyoandaliwa.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment