Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, 20 June 2017

OBASANJO AMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA USIMAMIZI WA UCHUMI

Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017
*******************
RAIS John Magufuli ameendelea kupokea pongezi kutoka ndani na nje ya Tanzania ambapo leo Rais Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo amempongeza kwa kuonesha mfano bora katika Bara la Afrika katika kusimamia uchumi na kutetea maslai ya nchi katika uwekezaji.

Rais Mstaafu Obasanjo ametoa pongezi hizo muda mfupi baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.

Obasanjo amesifu juhudi za Rais Magufuli kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali duniani na kusimamia ipasavyo sera ya kuhakikisha nchi inanufaika, badala ya kuacha wawekezaji wakijinufaisha wenyewe na nchi kuambulia kiasi kidogo cha mapato.

“Nimepita katika nchi kadhaa zikiwemo Msumbiji, Malawi na sasa nipo hapa Tanzania, na huko kote nazungumzia masuala ya uchumi na namna nchi zetu za Afrika zinapaswa kunufaika na uwekezaji katika maeneo mbalimbali.

“Uchumi wa Tanzania unakwenda vizuri sana, na juhudi za Rais Magufuli za kuhakikisha nchi yake inanufaika na uwekezaji ni suala muhimu sana na la mfano, ameonesha mfano mzuri kwa viongozi wa Afrika na hii ndio njia pekee itakayotuwezesha kukuza uchumi wetu, hatuwezi kuendelea kuwaacha wawekezaji wananufaika wao na sisi kuambulia kiasi kidogo sana” amesema Rais Mstaafu Obasanjo.

Wakati huo huo, Rais Magufuli ameridhia ombi la Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Mwendwa Judith Malecela kujiuzulu wadhifa wake.

Rais Magufuli ameridhia kujiuzulu kwa Mwendwa Judith Malecela kuanzia leo Juni 20, 2017.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment