Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday 19 June 2017

MFUMO WA USAJILI NCHINI KUBORESHWA

 Waziri wa Katiba na  Sheria Prof.  Palamagamba  Kabudi akizungumza.

Serikali ya Tanzania inafanya maboresho ya Mfumo wa Usajili uliopo na kuanzisha mfumo utakaofanya kazi vizuri usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu nchini unaofanywa na Wakala wa  Usajili, Ufilisi na Udhamini - RITA 
 
Waziri wa Katiba na  Sheria Prof.  Palamagamba  KABUDI amesema hayo mjini Dodoma wakati akifungua mkutano wa wadau wanaojadili mfumo huo.
 
Amesema maboresho ya mfumo huo yanatekelezwa kupitia Mkakati wa Kitaifa wa usajili wa Matukio muhimu ya binadamu na takwimu (Civil Registration and Vital Statistics(CRVS). 
 
Prof Kabudi amesema Mfumo huo unalenga kutatua changamoto mbalimbali ambazo zimefanya hali ya usajili wa Matukio muhimu ya binadamu kutokuwa ya kuridhisha nchini. 
 
Ameongeza kuwa ana imani kuwa utekelezaji wa mkakati huo itakuwa njia sahihi itakayowezesha kumuona kila mwananchi katika picha ya taifa.
 
Mkutano huo wa wadau wa usajili wa Matukio muhimu ya mwanadamu nchini umeandaliwa na RITA


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment