Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday 6 May 2017

SPIKA JOB NDUGAI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI AJALI ILIYOUWA 32 ARUSHA



SPIKA wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai amemtumia Salam za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Mrisho Gambo kufuatia vifo vya Wananfunzi 29, Walimu 3 na Dereva 1, wa Shule ya Msingi Lucky Vicent ya Mkoani Arusha, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali leo asubuhi katika eneo la Rhotia Marera, Wilayani Karatu Mkoani Arusha.

“Mhe Mkuu wa Mkoa nakupa pole sana, nimepokea kwa mshtuko taarifa hii ya ajali iliyogharimu maisha ya watoto wetu, hakika hili ni pigo kwa taifa zima, namuomba mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.” alisema Mheshimiwa Ndugai.

“Natoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao, Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu, vilevile Nnawaombea majeruhi wote wa ajali hiyo wapate uponyaji wa haraka” aliongeza Mheshimiwa Ndugai.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment