Home
About Us
Siasa
Uchumi
Biashara
Michezo
Burudani
Wasiliana Nasi
Have you got a good story?
Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.
Have you got a good story?
Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.
Saturday, 6 May 2017
NEC YATOA UFAFANUZI UTARATIBU WA KUMPATA MBUNGE NA DIWANI VITI MAALUM
Saturday, May 06, 2017
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza kuwa nafasi za Wabunge wa Viti Maalum wanaoteuliwa zipo kwa mujibu wa Sheria na zimeainishwa katika Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Akitoa ufafanuzi huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amesema kuwa Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba inaeleza utaratibu mzima wa kuwapata Wabunge wanawake wa Viti maalum.
Amesema kila Chama cha Siasa kinachoshiriki katika Uchaguzi Mkuu na kupata angalau asilimia 5 ya Kura zote halali za wabunge kitapata Wabunge wa Viti Maalum kulingana na Kura ambazo chama husika kimepata.
Amefafanua kuwa Chama kinachopata asilimia 5 ya Kura zote halali za Wabunge katika Uchaguzi Mkuu kinatakiwa kuwasilisha orodha ya wanachama wanaopendekezwa kuwa wagombea wa Viti Maalum ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Aidha, ameeleza kuwa endapo inatokea nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na sababu mbalimbali, Spika wa Bunge humtaarifu Mwenyekiti wa Tume juu ya uwepo wa nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.
Amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume hukiandikia barua chama husika kukitaarifu juu ya uwepo wa nafasi wazi ya viti maalum ili kiweze kuwasilisha pendekezo la jina katika orodha kiliyowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka 2015, ikiambatanishwa na Fomu namba 8 D ya kuomba jina lililopendekezwa liteuliwe na Tume katika nafasi ya Ubunge kulingana na sifa zilizoainishwa kwa mujibu wa Sheria.
Saturday, May 06, 2017
Copyright: Dailynews Blog
Mtumie Rafiki Yako
Maoni: 0
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Newer Post
Older Post
Home
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
Tags
Kumbu Kumbu
ELIZABETH MICHAEL AU LULU NINANI?
MUIGIZAJI na Muongozaji Filamu, Elizabeth Michael (Lulu) ,22, leo amehukumuiwa kifungo cha Miaka Miwili gerezani baada ya Mahaka Kuu Tan...
YALIYOJIRI MAGAZETI YA SERIKALI YA DAILY NEWS NA HABARI LEO JANUARI 18,2017
RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA BILL GATES NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa tasisi ya Bill and Melinda Gates Founda...
FOUR-DAY TRAINING FOR SOUTH SUDAN MEDIA PROFESSIONALS BEGINS IN ARUSHA
The Director of Infrastructure at the EAC Secretariat, Dr. Kamugisha Kazaura, officially opened the four-day Republic of South Sudan Me...
TANZANIA IMEMALIZA RASMI MUDA WAKE KUONGOZA KUNDI LA G77 NA CHINA KWA MWAKA MMOJA KATIKA UMOJA WA MATAIFA-GENEVA, USWISI
Balozi Dkt. James Alex Msekela akikabidhi uenyekiti wa Kundi la G77 na China Umoja wa Mataifa Geneva kwa Balozi. Farukh Amil wa Pakistani J...
MCHEZO WA M-BET WAMWAGA SHILINGI MILIONI 826
Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Kabora Mboya(kushoto)akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 109/- Mwanafu...
MKURUGENZI WA HAMIDU CITY PARK AFUTURISHA KIGAMBONI
Hamidu H. Mvungi miliki wa kijiji cha Hamidu City Park, Mikwambe Kibada Kigamboni chenye nyumba 1500 akizungumza na wageni waalikwa mba...
SIKIA HAPA ALICHOKISEMA RICHARD KAYOMBO KUHUSU ULIPAJI KODI ZA MAJENGO
VIONGOZI MKOA WA MBEYA WATAMBA KULIPIZA KISASI KWA VIONGOZI WA DINI
Kocha mchezaji wa timu ya Viongozi mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akionesha ufundi wake wa kutuliza mpira wakati akiwanoa wachezaji wake. ...
CHEGENI AANZA KUTOA TIBA YA VYUMA KUKAZA BUSEGA
MBUNGE wa Jimbo la Busega Dk. Raphael Chegeni akizungumza katika mkutano wa hadhara Na Mwandishi wetu MBUNGE wa Jimbo la Busega D...
Labels
BURUDANI
MICHEZO
SIASA
Kumbu Kumbu
January
(86)
February
(95)
March
(131)
April
(117)
May
(113)
June
(127)
July
(81)
August
(69)
September
(46)
October
(55)
November
(21)
December
(47)
January
(66)
February
(32)
March
(41)
April
(40)
May
(27)
June
(9)
October
(1)
BLOG MBALI MBALI
MICHUZI BLOG
TANZANIA KUANDAA WORLD TRAVEL AWARDS 2025 KWA BARA LA AFRIKA – DKT ABBASI
Father Kidevu
HIMAHIMA TUJITOKEZE KWA WINGI KUPIGA KURA 27 NOVEMBA 2024-KAPINGA
HABARI LEO
Arusha on spotlight
OFA YA MATANGAZO
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment