Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday, 1 May 2017

MKUU WA MKOA AOMBA USHIRIKIANO WA WAFANYAKAZI



Waalimu wa Shule mbali mbali za mkoani hapa wakiwa katika madhimisho ya Mei Mosi katika uwanja wa CCM Kirumba.
Wanafunzi wa shule ya ufundi ya Wavulana ya Bwiru wakiwa katika maadhimisho ya Mei Mosi katika uwanja wa CCM Kirumba
 *************
Na Alexander Sanga,Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amewaomba waajiri na waajiriwa wanahakikisha wanadumisha ushirikiano baina yao pamoja na serikali ili kuhakikisha wanaleta maendeleo nchini.

Akizungumza katika sherehe za kusherekea sikukuu ya Mei Mosi kimkoa iliyofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba katika wilaya ya Ilemela,Mongela alisema ushirikiano ukiwepo baina ya wafanyakazi utasaidia katika kutatua kero za wafanyakazi.

Mongela alikemea tabia ya wajiri kutoa hundi hewa wafanya bora pamoja na tabia ya ukopaji wa zawadi kwa wafanyakazi bora wa Mei mosi uachwe haraka.

‘’Nakemea sana tabia hii ya kukopa zawadi za washindi wa wafanyakazi bora jambo sio zuri kabisa,mfano mzuri ni ofisi yangu wale wafanya kazi bora wa mwaka jana hawakupewa zawadi zao wamekuja kupewa zawadi za mwaka jana leo asubuhi(Jumatatu)’’ Mongela alisema.

Mkuu wa mkoa aliagiza zawadi za wafanyakazi bora wa wilaya ya Sengerema na Misungwi wapewe zawadi zao za mwaka jana.Pia alipongeza kauli mbiu ya Mei mosi mwaka huu inayosema ‘’Uchumi wa Viwanda,Ulenge Kulinda haki na maslahi na heshima ya mfanyakazi’’.

Kwa mujibu wa Mongela alisema kauli mbiu hii ni muafaka kabisa katika kutengeneza Tanzania ya viwanda ili kuendana na kasi ya Mheshimiwa rais John Magufuli.

Mongela aliziagiza Halmashauri na wilaya zote mkoani hapa zihakikishe zinakaa mabaraza ya wafanyakazi ili kuhakikisha zinatatua kero mbali mbali za wafanyakazi wake.Mongela alisema Halmashauri zote zikae vikao hivyo vya mabaraza kabla ya Oktoba 30 mwaka huu.

Mratibu mkuu wa Mei Mosi mwaka huu mkoani hapa Meshack Sarota ameomba makampuni ya mbali mbali mkoani hapa yaache mambo ya kuchelewesha mishahara kwa wafanyakazi wao.

Sarota alimuomba mkuu wa mkoa mkoa kuhakikisha anatatua kero mbali mbali za wafanyakazi mkoani hapa ili mkoa uweze kupata maendleo.

Sarota ameipongeza serikali kwa kuwalipa walimu posho zao pale wanapoahama kutoka shule mmoja kwenda nyingine.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment