MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla leo ameongoza wafanyakazi wa mkoa wa Mbeya na Wananchi katika sherehe za wafanyakazi Mei Mosi mkoani humo.
Akizungumza baada ya kupokea maandamano ya wafanyakazi kutoka taasisi na kampuni mbalimbali mkoani humo Makalla alisema atahakikisha anashughulikia matatizo ya wafanykazi mkoani humo yaliyo katika ngazi ya mkoa na yale ya kisera atayawasilisha katika Wizara na Mamlaka husika kwa kutafutiwa ufumbuzi kwa wakati.
Asema serikali haitomuonea mfanyakazi yeyote katika uwajibishaji kwa kumchukulia hatua za kinidhamu bali serikali itazingatia sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi.
Aidha Makalla amewataka waajiri kuwasilisha michango ya wafanyakazi katika mifuko ya Hifadhi ya jamii kwa mujibu wa sheria.
Makalla amewakumbusha wafanyakazi pamoja na haki watimize wajibu wao kwa kufanya kazi kwa bidii.
Pia amewashuruku Wafanyakazi, Viongozi wa wafanyakazi kwa kushirikiana n serikali katika kushughulikia changamotoza wafanyakazi.
Wafanyakazi wakiandamana Mkoani Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla pamoja na viopngozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya na wa Vyama vya wafanyakazi wakiimba wimbo wa mshikamano wa ndoa.
Mmoja wa wafanyakazi bora akikabidhiwa zawadi ya ufanyakazi bora.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment