Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Thursday, 19 January 2017

RAIS MAGUFULI AWAPANGIA VITUO MABALOZI SITA YUMO, NCHIMBI, KAIRUKI, MSEKELA, FATMA, KIONDO NA MADAFA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Januari, 2017 amewateua Mabalozi watano kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja Mabalozi walioteuliwa na vituo vyao vya kazi kama ifuatavyo;

  1. Balozi Mbelwa Brighton Kairuki ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Beijing – China.
  2. Balozi George Kahema Madafa ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Rome – Italy.
  3. Balozi Emmanuel John Nchimbi ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Brasilia – Brazil.
  4. Balozi Fatma M. Rajab ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Doha- Qatar.
  5. Balozi Prof. Elizabeth Kiondo ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Ankara – Uturuki.
  6. Balozi Dkt. James Alex Msekela ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Geneva – Umoja wa Mataifa.

Mabalozi hawa wataapishwa kesho tarehe 20 Januari, 2017 saa 10:30 Jioni Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Muhidin Ally Mboweto kuwa Balozi.

Tarehe ya kuapishwa na kituo cha kazi cha Bw. Muhidin Ally Mboweto kitatangazwa baadaye.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment