Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 22 June 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA BAGAMOYO-- MSATA KM 64

 Rais Dk John Magufuli leo Juni 22, 2017, amezindua barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata yenye urefu wa Kilometa 64 na kuipongeza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na wote waliofanikisha ujenzi wa barabara hiyo ambayo inasaidia kutatua tatizo la msongamano wa magari katika barabara ya Chalinze – Dar es Salaam na inapita katika eneo la Bagamoyo ambalo litajengwa bandari mpya na eneo la viwanda.

Ujenzi wa barabara hiyo yenye madaraja makubwa matatu umegharimu Shilingi Bilioni 213 ikiwa ni fedha zilizotolewa na Serikali ya Tanzania.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Mama Salma Kikwete (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete , Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuweka jiwe la ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani




Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani

Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akisalimia kabla ya ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akizungumza kabla ya ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani



Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akielezea hatua za ujenzi wa Madaraja katika barabara ya Bagamoyo-Msata huku Rais Dkt. Magufuli akimsikiliza.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment