Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 19 January 2017

SERIKALI YAONYA WAWEKEZAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO

Na Mwandishi wetu, Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua wawekezaji wanaochochea migogoro katika wilaya ya Ngorongoro na kusababisha uvunjifu wa amani hivyo kuchangia kuzorota kwa shughuli za maendeleo.

Gambo ameyasema hayo katika ziara yake wilayani Ngorongoro inayolenga kutatua migogoro wa pori tengefu lenye ukumbwa wa kilomita za mraba elfu kumi na tano ambapo amekutana na wadau mbalimbali ikiwemo wawekezaji,wafugaji pamoja na viongozi wa kiserikali.

Amesema kuwa serikali itawaondoa wawekezaji wanaochochea migogoro na kuwagombanisha wananchi na serikali yao jambo ambalo halitafumbiwa macho

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka amesema kuwa wako baadhi ya watu wanaonufaika na migogoro hiyo hivyo kumalizika kwa migogoro hiyo kutaleta manufaa kwa wananchi wengi kuliko kunufaisha kundi la watu wachache

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo,Kilimo na Uvuvi  ambaye pia ni Mbunge wa Ngorongoro Wiliam Ole Nasha na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa  Arusha  Lekule Laizer wamesema kuwa utatuzi wa mgogoro huo utasaidia kuepusha migongano ya kimaslahi na kuchochea shughuli za kimaendeleo badala ya kutumia muda mwingi katika usuluhishi wa miigogoro hiyo

Mkuu wa Mkoa ameanza Ziara yake leo Wilayani Ngorongo na kesho atatembelea katika vijiji mbalimbali ikiwa ni katika juhudi za kutatua mgogoro wa pori tengefu katika wilaya hiyo.




Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment