Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Friday 20 January 2017

IRINGA YASEMA HAKUNA NJAA

Na: Jovina Bujulu – MAELEZO
SERIKALI mkoani Iringa imesema hakuna njaa kwa sababu msimu wa mwaka 2015/2016 walizalisha tani zaidi ya milioni 1.4 zikijumuisha mazao ya nafaka, mizizi na mazao jamii ya kunde.

Akizungumzia hali ya upatikanaji wa chakula mkoani humo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa baadhi ya wananchi wengi wamejawa na tama ndiyo maana wanauza chakula badala ya kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya familia zao.

“Kila kaya inatakiwa kuhakikisha ina chakula cha kutosha badala ya kukiuza, na wataalam wa chakula wataendelea kupita kila nyumba kuhimiza utuinzaji wa chakula sambamba na uwiano wa mahitaji halisi,” alisema Mama Masenza.

Aliongeza kuwa kwa sasa Mkoa huo una ziada ya mazao ya nafaka tani 756,369.92 na kunde tani 61,584.63.


Hata hivyo alitoa wito kwa baadhi ya wananchi kuthamini familia zao kwa kuhifadhi chakula badala ya kukiuza kwa tama zao za kupata fedha kirahisi.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment